Na Saleh Ally, Kigali
HALI ya hofu ilitanda juzi baada ya kiongozi mkubwa wa Yanga kuugua ghafla na kulazimika kukimbizwa hospitali ambako alilazwa.
Seif Ahmed ‘Seif Magari’ ambaye sasa ni mjumbe wa bodi ya wafadhili wa Yanga, aliugua ghafla na kuishiwa nguvu, hali iliyomlazimu akimbizwe hospitali hapa jijini Kigali.
Hali ya ugonjwa ilimkuta kiongozi huyo wakati akiwa chumbani kwake, mara moja alichukuliwa na kupelekwa hospitali ambako alilazwa na kutundikiwa dripu. Seif Magari alipumzishwa katika hospitali hiyo iliyopo katikati ya jiji hili kwa takribani saa sita kabla ya kuruhusiwa.
Akizungumza hospitalini hapo baada ya Championi Ijumaa kumtembelea, Seif Magari alisema: “Ghafla niliishiwa nguvu na kushindwa hata kutembea, nikalazimika kuwapigia simu wenzangu wakanileta hospitali, ila sasa nipo safi kabisa, nasubiri dripu hii iishe, hakuna sababu ya kuwa na hofu.”
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na mjumbe, Abdallah Bin Kleb ni kati ya watu waliokuwa hospitalini hapo kumjulia hali. Juzi jioni, Seif alitoka na alionekana akiwa salama salimini katika Hoteli ya Serena.

SOURCE: GAZETI LA CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment