Samatta mbele akichuana na Kolo Toure, wakati Taifa Stars ilipomenyana na Ivory Coast mwezi uliopita |
Na Prince Akbar
MABINGWA mara nne Afrika, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo wanacheza na mabingwa mara tano Afrika, Zamalek
ya Misiri katika mchezo wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mazembe, inayojivunia mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania,
Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’ inahitaji ushindi katika mchezo huo wa leo wa nyumbani
ili kurejesha matumaini ya ubingwa, baada ya awali kufungwa na Al Ahly ya Misri
mjini Cairo 2-1 kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Berekum Chelsea ya Ghana nyumbani,
Lubumbashi.
Mazembe yenye pointi moja hivi sasa, ikishinda leo moja kwa
moja itakuwa imerudi kwenye mbio za ubingwa wa Afrika, lakini matokeo tofauti
na ushindi yatawaweka njia panda.
Mechi nyingine ya kundi hilo leo ni kati ya Ahly inayoongoza
Kundi hilo kwa pointi zake sita, na Chelsea ya pili yenye pointi nne, mjini Cairo.
Zamalek haina pointi na inashika mkia jambo ambalo linaufanya mchezo wa leo Lubumbashi
kwenye Uwanja wa TPM uwe mgumu mno.
MSIMAMO WA KUNDI B LA AKINA SAMATTA AFRIKA:
KUNDI B
P W D L GF GA GD Pts
1 Al Ahly 2 2 0 0 3 1 2 6
2 Berekum Chelsea 2 1 1 0 5 4 1 4
3 TP Mazembe 2 0 1 1 3 4 -1 1
4 Zamalek 2 0 0 2 2 4 -2 0
MECHI ZA LEO AFRIKA:
TP Mazembe v Zamalek (Saa 10:30 jioni, Lubumbashi)
Al Ahly v Berekum Chelsea (Saa 5:00 usiku, Cairo)
0 comments:
Post a Comment