Sama Goal |
Na Prince Akbar
MABINGWA mara nne Afrika, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jioni hii wamefufua matumaini ya ubigwa wa tano
wa michuano hiyo, baada ya kuifunga Zamalek ya Misiri mabao 2-0 katika mchezo
wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa TPM, mjini
Lubumbashi.
Shukrani kwao, N. Kasongo aliyefunga bao la kwanza
dakika ya 70, akimalizia pasi ya D. Kanda na Mbwana Ally Samata aliyeongeza la
pili dakika ya 77, akiunganisha pasi Tressor Mabi Mputu.
Mazembe sasa imefikisha pointi nne, baada ya awali kufungwa
na Al Ahly ya Misri mjini Cairo 2-1 kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na
Berekum Chelsea ya Ghana nyumbani, Lubumbashi.
Mechi nyingine ya kundi hilo leo kati ya Ahly inayoongoza
Kundi hilo kwa pointi zake sita, na Chelsea ya pili yenye pointi nne, mjini
Cairo itachezwa baadaye saa 5:00 usiku. Zamalek haina pointi na inashika mkia.
MSIMAMO WA KUNDI B LA AKINA SAMATTA AFRIKA:
KUNDI B
P W D L GF GA GD Pts
1 Al Ahly 2 2 0 0 3 1 2 6
2 Berekum Chelsea 2 1 1 0 5 4 1 4
3 TP Mazembe 3 1 1 1 5 4 1 4
4 Zamalek 3 0 0 3 2 6 -4 0
MECHI NYINGINE LEO AFRIKA:
Al Ahly v Berekum Chelsea (Saa 5:00 usiku, Cairo)
0 comments:
Post a Comment