Real wakiwa na Super Cup Cup yao
Ronaldo
|
Higuain |
MADRID,
Hispania
KLABU
ya Real Madrid imetwaa taji lake la kwanza la Super Cup ya Hispania ndani ya
miaka minne kufuatia mabao ya Gonzalo Higuain na Cristiano Ronaldo kuwapa
ushindi wa 2-1 dhidi ya Barcelona waliomaliza mechi wakiwa 10 usiku wa kuamkia
leo.
Ushindi
huo dhidi ya Barca, iliyompoteza Adriano aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu
dakika ya 28 tu ya mchezo huo, ulifanya matokeo ya jumla ya mechi mbili za
kuwania taji hilo, yawe 4-4, baada ya Wakatalunya hao kushinda 3-2 katika mechi
ya kwanza Uwanja wa Nou Camp na Real wakapewa taji kwa sheria ya mabao ya ugenini.
Kocha
Mreno, Jose Mourinho aliinuka kushangilia mabao yote ndani ya dakika 20 tu za
mwanzo, la kwanza dakika ya 11 kwenye Uwanja wa Bernabeu, mfungaji Higuain akitumia
mwanya wa makosa ya safu ya ulinzi ya Barca na dakika na dakika nane baadaye
Ronaldo akafunga la ushindi.
Lionel
Messi aliifungia Barca bao la kufutia machozi kabla ya mapumziko kwa mpira wa adhabu,
akifumua shuti kutoka umbali wa mita 30.
Pedro
aliokolewa mchomo mmoja mkali sana na Iker Casillas dakika 30 kuelekea mwisho
wa mechi hiyo na timu zote zilipata nafasi za kuongeza mabao, lakini bahati
ilikuwa upande wa Real jana kumaliza ubabe wa miaka mitatu mfululizo wa Barca
katika taji hilo.
Mechi
hiyo ilifufua matumaini na furaha ya kikosi cha Mourinho, ambacho kilipoteza
mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Hispania, La Liga kwa kufungwa 2-1 na Getafe
Jumapili.
(Imeandikwa
na Iain Rogers, imetafsiriwa na Mahmoud Zubeiry)
0 comments:
Post a Comment