Mudde kulia |
Na Prince
Akbar
SIMBA imetema kiungo Mganda, Mussa Mudde katika usajili wake, kwa
sababu imegundulika, majeruhi yake yatamuweka nje ya Uwanja kwa muda mrefu na
badala yake imemsajili beki kutoka Mali, Komabil Keita.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema
jioni hii kwamba, Mudde atakuwa nje ya Uwanja kwa miezi mitatu hivyo hataweza
kucheza kabisa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu na kwa sababu hiyo anaondolewa na
nafasi yake anapewa Keita.
Tayari Keita yupo na Simba kambini mjini Arusha na ingawa jana katika
mechi ya kirafiki dhidi ya Mathare United, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini
Arusha aliumia na kutoka nje Wekundu wa Msimbazi wakishinda 2-1, lakini imeelezwa
leo alifanya mazoezi na wenzake.
Kwa marekebisho hayo, wachezaji wa kigeni wa Simba SC wanakuwa ni
Keita, Emmanuel Okwi kutoka Uganda, Daniel Akuffo kutoka Ghana, Felix Sunzu
kutoka Zambia na Paschal Ochieng kutoka Kenya.
Aidha, Mudde anakuwa mchezaji wa kigeni wa tatu kusajiliwa kwa ajili
ya msimu ujao na kutemwa kabla ya kuanza kazi, wengine wakiwa ni Lino Masombo
na Kanu Mbivayanga, wote kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
0 comments:
Post a Comment