Mbuyu Twite |
Na
Mahmoud Zubeiry
ALHAJ Ismail Aden Rage, yupo njiani kurejea Dar es
Salaam ‘kishujaa’, akitokea Kigali, Rwanda baada ya kukamilisha usajili wa beki
wa APR ya nchini humo, Mbuyu Twite hii leo.
Habari za ndani kutoka Simba SC, zimesema kwamba Simba
imemsainisha Twite, mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh. Milioni 50,
akitanguliziwa Milioni 30 na nyingine atapewa baadaye.
Twite atakuwa akilipwa Sh. Milioni 2 mshahara kwa
mwezi, sawa na Mrisho Ngassa aliyesajiliwa leo rasmi kutoka Azam.
APR hawajapata senti tano nyekundu katika uhamisho wa
beki huyo wa Amavubi, kwa kuwa amemaliza mkataba wake mwezi huu jeshini.
Simba imekubaliana na ndugu yake Mbuyu, kiungo Kabange
Twite kuingia naye mkataba Desemba mwaka huu, akimaliza mkataba wake na APR.
0 comments:
Post a Comment