Jioni ya leo, BIN
ZUBEIRY alitembelea kambi ya mazoezi ya kikosi cha pili cha Yanga, na kuwakuta wachezaji wa timu hiyo
wakinolewa na makocha wao, wachezaji wa zamani wa timu hiyo, Salvatory Edward ‘Doctor’
na Abubakar Salum ‘Sure Boy’ Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam.
Kivutio alikuwa ni
kinda wa umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi
Lumumba, Suleiman Abdallah Kahera, maarufu kama Okwi mbele ya wachezaji wenzake
akifananishwa na mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi kiuchezaji. Dogo anayecheza wingi ya kushoto anajua
na kama atapata malezi mazuri kisoka, miaka mitano ijayo, atakuwa habari
nyingine. Ana kasi, uwezo wa kumiliki mpira, kuuchezea na kupiga chenga za
kusisimua. Tazama picha za mazoezi hayo leo.
|
Wachezaji wakisikiliza maelekezo ya walimu wao kulia |
|
Anayetabasamu kulia mbele ni Okwi wa Yanga B |
|
Makocha Salvatory Edward kulia na Sure Boy kushoto |
|
Mazoezi ya kuchezea mpira |
|
Dogo Okwi akifanya mambo |
|
Kocha Salvatory akiwafundisha kwa mifano |
|
Dogo Okwi kushoto ananyoosha viungo |
0 comments:
Post a Comment