WA HAPA HAPA; Okwi amekwama Ausrtia, anarudi Dar |
Na Mahmoud Zubeiry
SIJUI imekuwaje, lakini habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata
mida hii, ni kwamba, klabu ya FC Red Bull Salzburg ya Wals-Siezenheim, Austria haitamnunua
tena mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Arnold Okwi, licha ya awali kuelezwa
kwamba amefuzu majaribio katika klabu hiyo, baada ya wiki tatu za kuwa nchini
humo akijaribiwa.
Chanzo cha habari kutoka Simba kimesema kwamba, Okwi
amekwama na anarejea Simba SC, lakini wakati huo huo, habari ambazo zimeenea
mjini, katika kulipa kisasi cha kumkosa Mrisho Khalfan Ngassa, Mwenyekiti wa
Yanga, Yussuf Mehboob Manji anaisaka saini ya Okwi kwa gharama yoyote.
Hivi sasa Okwi yuko tayari Uganda, baada ya kurejea kutoka
Austria, akidai amerudi kujitibu Malaria.
Jana, Katibu wa Simba Evodius Mtawala aliiambia BIN
ZUBEIRY kwamba; “Okwi amefuzu majaribio, ila ana Malaria, amekuja
kuitibu kasha anarudi Austria kwa ajili ya vipimo,”alisema Mtawala.
Kukwama kwa Okwi kunaikosesha Simba Euro 600,000 ambazo
klabu hiyo, ilikuwa tayari kutoa.
Awali, Simba ilipata ofa ya kumuuza Okwi kwa Sh. Bilioni 2 kwa
klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, lakini mshambuliaji huyo akasema
anataka kwenda Ulaya.
Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi
akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya
kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.
Wakati huo huo, habari nyingine ambazo zinatikisa Jiji kwa
sasa ni Said Bahanuzi ‘Spider Man’ kusaini Simba, lakini BIN ZUBEIRY imezungumza
na mfungaji huyo bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame, na akasema; “Sina tatizo na Yanga, mimi mchezaji halali wa Yanga, na
sina mpango wa kwenda Simba kwa sasa, huo ni uzushi kaka,”alisema.
0 comments:
Post a Comment