Okwi |
Na Mahmoud Zubeiry
EMMANUEL Okwi, mshambuliaji wa Simba SC amefuzu majaribio
katika klabu ya FC Red Bull Salzburg ya Wals-Siezenheim, Austria baada ya wiki
tatu za kuwa nchini humo akijaribiwa.
Katibu wa Simba Evodius Mtawala ameiambia BIN
ZUBEIRY sasa hivi; “Okwi amefuzu majaribio, ila ana malaria, amekuja
kuitibu kasha anarudi Austria kwa ajili ya vipimo,”alisema Mtawala.
Iwapo Okwi atafuzu kwenye vipimo vya afya, Simba itavuna
Euro 600,000 za mauzo ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugandfa.
Klabu hiyo inayotumia Uwanja wa Red Bull Arena, ikiwa zaidi
inafahamika kama SV Austria Salzburg kabla haijanunuliwa na kampuni ya Red Bull
mwaka 2005, imewahi kufika Fainali ya Kombe la UEFA mwaka 1994 na inacheza Ligi
Kuu ya Austria, iitwayo Bundesliga kama Ligi Kuu ya Ujerumani.
Timu hiyo ni kama timu ambayo Okwi, anachezea kwa sasa,
Simba SC, kwani nayo inavaa jezi za rangi ya nyeupe na nyekundu na imewahi kutwaa
taji la Bundesliga ya Austria mara saba na pia ilicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya
msimu wa 1994–1995 kama Casino Salzburg, na kuwa timu pekee, ambayo haikufungwa
na mabingwa wa wakati huo, Ajax Amsterdam.
Awali, Simba ilipata ofa ya kumuuza Okwi kwa Sh. Bilioni 2 kwa
klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, lakini mshambuliaji huyo akasema
anataka kwenda Ulaya.
Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi
akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya
kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.
0 comments:
Post a Comment