|
Kaburu akimkabidhi Ngassa jezi |
|
Ngassa akiwasili kama unavyoona umati unamlaki |
|
Kaburu akizungumza, kushoto Ngassa |
|
Meneja Vifaa wa Simba SC, Kessy Rajab akiwa nyuma ya Ngassa |
|
Ngassa |
|
Ngassa |
|
Ngassa |
|
Waandishi, Asha Kigundula na Dina Ismail kulia |
|
Mwandishi Somoe Ng'itu |
|
Ngassa anavaa jezi |
|
Imempendezaje? |
|
M16 wa Msimbazi |
|
TABASAMU; Kijana anafurahia maisha mapya |
|
KARIBU SANA; Kaburu akipeana mikono na Ngassa baada ya kusaini |
|
Kaburu akimuangalia Ngassa wakati anazungumza |
|
MISHA POPOTE; Ngassa leo yuko Simba |
|
AAHIDI MATAJI; Anasema anataka kushinda mataji na Simba |
Na
Mahmoud Zubeiry
MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Iric Nyange ‘Kaburu’,
majira ya saa 5:00 asubuhi ya leo, amemtambulisha kiungo mshambuliaji mpya wa
klabu hiyo, Mrisho Khalfan Ngassa ambaye alisajiliwa rasmi jana kwa dau la
jumla la Sh. Milioni 55, kutoka klabu ya Azam FC, akisaini mkataba wa miaka miwili.
Ngassa alipokewa kwa shangwe makao makuu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi na
mamia ya mashabiki wa klabu hiyo, na kuingizwa kwenye ukumbi wa mikutano
kutambulishwa rasmi. Tendo bila kuchelewa, katika ukumbi uliosheheni Waandishi
wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, ‘Mr Liverpool’, Ezekiel
Kamwaga, Ofisa Habari wa Simba SC alimkaribisha Nyange Kaburu amtambulishe Ngassa.
Pamoja na kuzungumzia Mkutano Mkuu wa Simba,
utakaofanyika Jumapili katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, Kaburu alimtambulisha
Ngassa na kumkabidhi jezi namba 16, ambayo alikuwa anaivaa Azam.
Ngassa alisema kwamba anashukuru kwa mapokezi mazuri
Simba SC, yamemfariji na sasa wana Simba wasubiri kulipwa fadhila zao. “Naamini
tu nitafanya vizuri katika klabu hii, kushinda mataji na Simba ndio ndoto
zangu, namshukuru Mungu. Hii ni klabu kubwa, klabu ambayo hata baba yangu aliichezea,”alisema
Ngassa.
Simba ilifanikiwa kumalizana na Ngassa jana na
kusaini naye mkataba wa miaka miwili, ambao umemfanya aondoke na zaidi ya Sh.
Milioni 35, Milioni 12 akipewa taslimu na nyingine akipewa gari (Milioni 18),
wakati mpenzi mwingine wa Simba amemuongezea Milioni 5.
Katika mkataba huo wa Simba na Ngassa, mshambuliaji
huyo atakuwa akilipwa Sh. Milioni 2 mshahara kwa mwezi, Milioni 1 ipo kwenye fomu
ya mkataba na Milioni 1 atakuwa akiongezewa na mtu.
Usajili wa mchezaji huyo, ulikakamilishwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Hans Pop, ambaye ndiye alitoa
fedha hizo na baada ya kumsainisha na kumkabidhi haki yake, ili kumuondolea
usumbufu akambadilishia ‘chipu’ ya simu, ili akina Seif Magari wasimpate.
Juzi Simba ilimnunua Ngassa kutoka Azam kwa Sh.
Milioni 25, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Yanga akagoma kwa sababu
hakushirikishwa katika dili hilo.
Kwa kumuongeza ‘kifurushi’ cha Sh. Milioni 35, ina
maana Simba imemsajili Ngassa kwa Sh. Milioni 60 kwa miaka miwili, ambalo ni
dau kubwa zaidi la usajili kwa mchezaji huyo tangu aanze kucheza soka.
Yanga ilimsaini kwa Sh. Milioni 25 jumla kutoka
Kagera Sugar mwaka 2007 pamoja na uhamisho wake akasaini mkataba wa miaka
mitatu, wakati miaka miwili iliyopita, Azam ilimsajili kwa Sh. Milioni 55
pamoja na uhamisho wake (Sh. Milioni 30) ikimsainisha mkataba wa miaka mitatu,
ambao ulitarajiwa kumalizika mwakani.
Azam ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya
mchezaji huyo iliyemsajili kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya
Yanga baada ya kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC).
Na uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim Bakhresa
mwenyewe, ambaye alikerwa na kitendo hicho akawaagiza wanawe, Wakurugenzi wa
bodi ya timu wamuuze mchezaji huyo popote, haraka iwezekanavyo.
0 comments:
Post a Comment