Kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime |
Na Prince Akbar
SHIRIKISHO
la Soka Uganda (FUFA) limetuma Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya
mchezaji Ayoub Hassan Isiko aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea timu ya Bull
FC ya nchini humo.
ITC
hiyo ilitumwa jana (Agosti 30 mwaka huu), hivyo kufanya wachezaji ambao ITC
hazijapatikana hadi sasa kubaki wawili tu. Dirisha la usajili wa wachezaji
litafungwa rasmi Septemba 4 mwaka huu.
Wachezaji
ambao ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng kutoka AFC
Leopards ya Kenya waliojiunga na Simba. ITC hizo zinatarajiwa kupatikana wakati
wowote kwani tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshaziomba
kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) baada ya nyaraka zote zilizokuwa
zikitakiwa kupatikana.
0 comments:
Post a Comment