Kushoto ni Mtakatifu Tom na kulia ni jamaa gani sijui |
Na Prince Akbar
KOCHA wa klabu bingwa soka ya Afrika Mashariki na
Kati, Yanga SC, Mbelgiji Tom Saintefiet amesema kwamba tangu amejiunga na klabu
hiyo mwezi uliopita hajawahi kuomba kazi sehemu nyingine yoyote.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Mtakatifu Tom
amesema anashangazwa mno na habari hizo za kizushi, za kizandiki zenye kulenga
kumchonganisha yeye na mwajiri wake, Yanga SC.
“Nakumbuka niliwahi kuomba kazi Chama cha Soka Kenya (KFF) kufundisha timu yao ya
taifa (Harambee Strars), lakini ilikuwa ni muda mrefu sana hata kabla sijaomba kazi
Yanga,”alisema kocha huyo aliyeipa Yanga ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame Jumamosi, akiifunga Azam FC 2-0.
Blog moja iliyowahi kuandika Iddi Kipingu anagombea
Uenyekiti Yanga, leo imeandika habari yenye kichwa kisemacho; “WIKI MOJA BAADA
YA KUIPA UBINGWA: KOCHA WA YANGA TOM SAINTFIET ATUMA MAOMBI YA KUIFUNDISHA
HARAMBEE STARS,”.
Akiizungumzia habari hiyo, Mtakatifu Tom alisema; “Ni uongo,
tangu nimesaini mkataba na Yanga, sijawahi kuomba kazi pengine popote,”alisema.
0 comments:
Post a Comment