// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MKUTANO SIMBA LEO, NGASSA MBUYU TWITE WARAHISISHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MKUTANO SIMBA LEO, NGASSA MBUYU TWITE WARAHISISHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 05, 2012

    MKUTANO SIMBA LEO, NGASSA MBUYU TWITE WARAHISISHA

    Mrisho Ngassa kushoto na Uhuru Suleiman kwenye mazoezi ya Simba. Picha na Salehe Ally.

    Na Princess Asia
    MKUTANO Mkuu wa mwaka wa klabu bingwa ya soka Tanzania, Simba SC unatarajiwa kufanyika leo, katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam, ajenda kuu zikiwa ni tatu.
    Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Iric Nyange ‘Kaburu’ alisema jana alipozungumza na BIN ZUBEIRY kwamba ajenda kuu itakuwa ni taarifa ya Mapato na Matumizi, Taarifa ya Mafanikio ya msimu na Kuelekea msimu ujao, ambao Simba itacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu ya Bara.
    Katika taarifa ya mapato na matumizi, bila shaka wanachama wa Simba wataambiwa ni kiasi gani cha fedha kilipatikana kutokana na mapato ya milangoni, mikataba ya udhamini ya Kilimanjaro Beer na Push Mobile na wafadhili wengine, kama Zakaria Hans Pop aliyefanikiwa usajili wa wachezaji kadhaa, wakiwemo Felix Sunzu na Mrisho Ngassa.
    Aidha, wanachama wa Simba watatarajia pia kuelezwa kuhusu mauzo ya wachezaji Mbwana Samatta na Patrick Ochan kwenda Tout Puissant Mazembe na Mussa Hassan Mgosi kwenda Daring Club Motema Pembe, zote za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Aidha, wanachama wa Simba watatarajiwa kuambiwa rasmi juu ya usajili wa wachezaji wapya, wakiwemo Mrisho Ngassa kutoka Azam FC na Mbuyu Twite kutoka APR ya Rwanda.
    Lakini pia watatarajia kupewa undani wa sakata la beki Kelvin Yondan, kusaini mkataba wa klabu hiyo na kwenda kusaini pia Yanga ambako amejiunga nao rasmi na amekwishaanza kuwachezea na tayari amesherehekea nao taji la kwanza, Kombe la Kagame mwezi uliopita.
    Mkutano wa leo, ni mwanzo pia wa Wiki ya Simba na Jamii, ambayo Kaburu alisema itahusu wachezaji, viongozi na walimu wa timu hiyo kufanya ziara sehemu mbalimbali za kijamii, kama hospitali, vituo vya watoto wa yatima, shule za msingi na kiwanda cha TBL, wadhamini wao wakuu.
    Kaburu pia alikumbushia kuhusu tamasha la kila mwaka la Simba SC, Simba Day, ambalo na mwaka huu tena litafanyika Agosti 8, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. “Maandalizi ya Simba Day yamekwishaanza na yanaendelea vizuri na kwa sasa kocha yupo kwenye harakati za kuboresha timu,”alisema Kaburu.
    Maandalizi ya Mkutano wa leo hapana shaka yatakuwa mazuri, kwa sababu Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), iliwakabidhi Simba SC Sh. Milioni 20 kwa ajili ya Mkutano huo, ikiwa ni sehemu ya makubaliano baina ya pande hizo katika mkataba wao wa udhamini.

    RATIBA YA WIKI YA SIMBA NA JAMII:
    Agosti 5, 2012: Mkutano Mkuu wa mwaka Simba SC (Polisi Oystrebay)
    Agosti 6, 2012: Kutembelea watoto yatima Maungu Orphanage Center, K’ndoni Mkwajuni
    Agosti 7, 2012: Kutembelea wagonjwa Mwananyamala hospitali
    Agosti 8, 2012: Simba Day (Uwanja wa Taifa, burudani na mechi)
    Agosti 9, 2012: Kutembelea shule ya msingi Mgulani kuhamasisha michezo mashuleni
    Agosti 10, 2012: Kutembelea kiwanda cha TBL Ilala
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKUTANO SIMBA LEO, NGASSA MBUYU TWITE WARAHISISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top