Bin Kleb |
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah
Ahmad Bin Kleb yupo Kigali, Rwanda na jana alionekana kwenye kambi ya APR-
dhahiri anataka kusajili mchezaji mpya kutoka klabu hiyo.
Huyu Bin Kleb ndiye aliyemsajili Haruna Hakizimana
Fadhil Niyonzima Yanga kutoka APR msimu uliopita na dhahiri kuwapo kwake katika
kambi ya APR si bure. Mapema mwezi uliopita, kulikuwa kuna habari, Yanga
inataka kumsajili mshambuliaji wa APR, Olivier Karekezi.
Lakini habari hizo zilipungua nguvu kutokana na
mchezaji huyo kushindwa kung’ara kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame mwezi uliopita.
Tayari Alhaj Ismail Aden Rage, yupo njiani kurejea
Dar es Salaam ‘kishujaa’, akitokea Kigali, Rwanda baada ya kukamilisha usajili
wa beki wa APR, Mbuyu Twite jana.
Habari za ndani kutoka Simba SC, zilisema jana kwamba
Simba imemsainisha Twite, mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh. Milioni
50, akitanguliziwa Milioni 30 na nyingine atapewa baadaye.
Twite atakuwa akilipwa Sh. Milioni 2 mshahara kwa
mwezi, sawa na Mrisho Ngassa aliyesajiliwa jana rasmi kutoka Azam.
APR hawajapata senti tano nyekundu katika uhamisho
wa beki huyo wa Amavubi, kwa kuwa amemaliza mkataba wake mwezi huu jeshini.
Simba imekubaliana na ndugu yake Mbuyu, kiungo Kabange
Twite kuingia naye mkataba Desemba mwaka huu, akimaliza mkataba wake na APR.
0 comments:
Post a Comment