Na Prince Akbar
MICHUANO ya BancABC Super 8 leo imeanza katika sura ya
kutopendeza, mjini Arusha mechi kati ya Polisi Morogoro na Mtibwa Sugar
ikishindwa kufanyika kwa sababu ya Menejimenti ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
kudai kutokuwa na taarifa za mashindano hayo, wakati Dar es Salaam Simba
ilichezesha timu B.
Simba B imetoka sare ya 1-1 na Jamhuri ya Pemba kwenye
Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam. Jamhuri ndio waliotangulia kupata bao
kupitia kwa Bakari Khamis dakika ya 48, akiunganisha krosi ya Abdallah Othman, kabla
ya Shomary Kapombe, mchezaji pekee wa Simba A aliyecheza, kuisawazishia timu
yake kwa penalti dakika ya 83, baada ya Miraj Adam kuangushwa kwenye eneo la
hatari na Mfaume Shaaban.
Michuano hiyo ina makundi
mawili, ikishirikisha timu nane, Kundi A likiwa na timu za Simba, Jamhuri,
Zimamoto na Mtende FC, wakati Kundi B kuna Super Falcon, Azam FC, Mtibwa Sugar
na Polisi Moro na bingwa wa michuano
hiyo inayodhaminiwa na Bank ABC ataondoka na Sh. milioni 40, mshindi wa pili
Sh. milioni 20, wa tatu Sh. milioni 15 sawa na wa nne, wakati washiriki wengine
wataondoka na Sh. Milioni 5 kila moja.
Michuano itachezwa katika vituo vinne vya Dar es Salaam,
Zanzibar, Arusha na Mwanza, ambapo timu zitasafirishwa kwa ndege kwenda kucheza
mechi katika vituo vyote. Kila timu itacheza mechi mechi katika vituo vituo
vitatu tofauti. Simba baada ya mechi ya leo, itakwea pipa kwenda Arusha kucheza
dhidi ya Mtende FC Alhamisi na itasafiri kwenda Mwanza kwa ajili ya mechi yao
ya mwisho ya Kundi A dhidi ya Zimamoto Jumamosi.
Wakati huo huo:
Mchezo wa tatu wa michuuano hiyo kati ya wenyeji Super Falcon imefungwa
nyumbani na Azam FC 2-0.
Gorikipa wa Jamhuri ya Permba, Jaffari Said akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Super 8 kwenye uwanja wa Chamazi jijini Dar.
Hassan Khatib akimiliki mpira
Beki wa Simba, Hassan Khatib akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Jamhuri ya Pemba, Mohamed Ally.
Mshambuliaji wa timu ya Jamhuri ya Pemba, Mohamed Ally akimtoka beki wa Simba, Hassan Khatib wakati wa mchezo wa Super 8 uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Timu hizo zilifungana 1-1. PICHA ZOTE NA HABARI MSETO BLOG
0 comments:
Post a Comment