Baada ya kuapishwa, viongozi wa Yanga walifanya kikao cha
Kamati ya Utendaji, ambacho kilifikia uamuzi wa kuvunja Kamati zote ndogondogo
ili kuunda Kamati mpya. Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji alisema Kamati ambayo
haitaguswa ni Kamati ya Uchaguzi pekee, iliyo chini ya Mwenyekiti Jaji John
Mkwawa.
Baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji, Manji alifanya kikao
kingine kidogo na wanachama, akiwa na Makamu wake, Clement Sanga. Kutoka hapo,
Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa akaenda kuzungumza na Waandishi wa Habari,
kuwapa yaliyofikiwa kwenye Kamati ya Utendaji.
Waliohudhuria kikao cha Kamati ya Utendajii,
pamoja na Mwenyekiti na Makamu wake, wengine ni Wajumbe wa Kamati hiyo, George
Manyama, Aaron Nyanda, Mohamed Bhinda, Titus Osoro, Sarah Ramadhan na Mussa
Katabaro. Alikosekana Abdallah Bin Kleb pekee, ambaye yupo Kigali, Rwanda kwa
majukumu ya klabu.
|
Kikao cha Kamati Utendaji |
|
Mwesigwa anazungumza na Waandishi |
|
Manji |
|
Manji na Sanga |
|
Manji na Sanga |
|
Manji na Sanga |
|
Manji katikati akizungumza na Waandishi, kulia Katibu Mwesigwa na kushoto Sanga |
|
Manji katikati, kulia Mwesigwa na kushoto Sanga |
|
Manji akizungumza na wanachama |
|
Wanachama wakimsikiliza Manji, wengine wakiandika kabisa anayozungumza ili kuweka kumbukumbu |
0 comments:
Post a Comment