Kutoka kushoto Mussa Katabaro, Clement Sanga, Abdallah Bin Kleb na Lameck Nyambaya, ambaye alianguka kwenye uchaguzi |
Na Prince Akbar
UONGOZI mpya wa klabu ya Yanga, chini ya Mwenyekiti wake,
Yussuf Mehboob Manji, unatarajiwa kutambulishwa rasmi mbele ya Mjumbe wa Baraza
la Wadhamini la klabu hiyo na Mlezi wa klabu hiyo, Mama Fatuma Karume, makao
makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kuanzia
saa 4:00 asubuhi leo.
Baada ya hapo, Wachezaji na viongozi wa Yanga watasafiri
kwenda Dodoma, kwa ajili ya mwaliko wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wapenzi wa klabu hiyo, Jumatatu.
Manji |
Wabunge hao, wamewaalika wachezaji wa Yanga, baada ya kutwaa
taji la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, kwa
mara ya pili mfululizo Jumamosi iliyopita, wakiifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye
fainali, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Julai 15, mwaka huu, Yanga ilipata viongozi wapya, ambao ni
Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu wake, Clement Sanga na Wajumbe wanne wa Kamati
ya Utendaji, Abdallah Bin Kleb, George Manyama na Mussa Katabaro.
Hao wanaungana na Wajumbe wengine waliosalia kutoka uongozi
uliochaguliwa mwaka juzi, Mohamed Bhinda, Titto Osoro, Salim Rupia na Sarah
Ramadhan, baada ya wajumbe wengine, wakiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga
na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu.
0 comments:
Post a Comment