Tetesi za Jumamosi magazeti ya Ulaya
MAN CITY, MAN UNITED ZAKAMATA VIFAA VYA NGUVU DAKIKA ZA LALA SALAMA
Manchester City inajipanga kuanza rasmi harakati za kumsajili kwa dau la pauni Milioni 20, kiungo wa kimataifa wa Roma, Daniele De Rossi, mwenye umri wa miaka 29.
Robin van Persie bado hayuko tayari kurejea Arsenal, baada ya Manchester United, Manchester City na Juventus kupunguza harakati zake za kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28.
Jose Mourinho amewaambia Arsenal hatawaunga mkono katika mpango wao wa kutaka kumsajili kiungo Nuri Sahin, mwenye umri wa miaka 23, kwa mkopo kutoka Real Madrid.
Manchester United ni kama imekamilisha uhamisho wa pauni Milioni 30 wa Mbrazil, Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, anayetokea Sao Paulo.
Liverpool na Tottenham Hotspur zote zinamfukuzia winga mwenye umri wa miaka 20 wa FC Porto, Christian Atsu, ambaye aliifungia bao lake la kwanza Ghana, Juni, mwaka huu.
Newcastle have made an enquiry for French midfielder Jeremy Toulalan, 28, currently with financially troubled Malaga.
Tottenham inaelekea kumkosa mshambuliaji wa Malaga, kutoka Venezuela, Salomon Rondon baada ya Rubin Kazan ya Urusi, kutoa ofa ya pauni Milioni 10.
Cardiff City imeanza mazungumzo ya kumsajili Craig Bellamy kutoka Liverpool, kiasi cha mwaka mmoja baada ya kumaliza kucheza kwa mkopo kusini mwa Wales.
Steve Pienaar anataka Everton imalizane na Manchester United kuhusu beki wa kushoto. Leighton Baines.
Wigan inataka kumchukua Mjapan wa Arsenal, mshambuliaji Ryo Miyaichi, mwenye umri wa miaka 19, kwa mkopo kama mbadala wa Victor Moses, anayeelekea kujiunga na Chelsea.
Manchester United inaelekea kuzipiga bao Chelsea na Juventus katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 23.
RODGERS ATAKA SUAREZ, EVRA WAMALIZE BIFU LAO
Brendan Rodgers anataka mshambuliaji wa Liverpool, Luiz Suarez kuachana na 'bifu' na Patrice Evra wa mahasimu wao, Man United.
0 comments:
Post a Comment