Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya
LIVERPOOL YAUZA WAWILI KUMNUNUA MPACHIKA MABAO MMOJA WA CHELSEA
Liverpool inamtaka mshambuliaji wa Chelsea, Daniel Sturridge na itawauza viungo Charlie Adam na Stewart Downing kukusanya fedha za kumnunua mchezaji huyo.
Kiungo wa Liverpool, Joe Cole anaweza kurejea West Ham kabla ya dirisha la usajili kufrungwa.
Manchester City ipo karibu kuinasa saini ya kinda wa umri wa miaka 19 wa Fiorentina, beki Mserbia, Matija Nastasic, na wao wakimtoa beki wa Montenegro, Stefan Savic pamoja na fedha kwenda upande wa pili.
QPR iko mbioni kukamilisha usajili wa kipa Mbrazil, Julio Cesar kutoka Inter Milan.
Tottenham inatumai kukamilisha usajili wa wachezaji watatu, Moussa Dembele kutoka Fulham, kipa wa Lyon, Hugo Lloris na mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk, Willian.
Mshambuliaji wa Genk mwenye umri wa miaka , Christian Benteke anatakiwa mno na Aston Villa.
Sunderland ina matumaini ya kuipiga bao Liverpool katika vita ya kuwania saini ya mshambuliaji Clint Dempsey baada ya kufanya mazungumzo na Fulham juu ya uhamisho wake.
Barcelona wiki hii itafungua milango ya kuondoka kwa winga wake Mholanzi, Ibrahim Afellay, ambaye Arsenal na Tottenham zinamtaka.
Everton inamtaka mshambuliaji wa bei mbaya wa Dundee United, Johnny Russell mwenye umri wa miaka 22.
AVB NA MOURINHO SASA SHWARI
Uhusiano mpya wa Tottenham na Real Madrid utawafanya makocha Andre Villas-Boas na Jose Mourinho kufanya kazi pamoja baada ya taarifa ya kuhitilafiana kwa miaka kadhaa.
Liverpool inahofia kiungo Mbrazil, Lucas Leiva, ambaye alikosa miezi sita msimu uliopita kwa maumivu ya goti, anaweza kuwa nje tena kwa miezi miwili kwa maumivu zaidi.
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amewapiga marufuku nyota chipukizi wa klabu yake, kuendesha gari za kimichezo kutoka kwa wadhamini wao wapya, Chevrolet.
0 comments:
Post a Comment