Tetesi za Jumamosi magazeti Ulaya


KINDA LA UFARANSA LAZIRUKA ARSENAL, AC MILAN, SPURS KUELEKEA EVERTON

Kocha wa Everton, David Moyes anataka kumsajili kinda wa umri wa miaka 17, Mfaransa M'Baye Niang kwa dau la pauni Milioni 2 kutoka Caen.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Daniel Sturridge ikiwa Andy Carroll ataondoka Anfield katika siku chache zijazo.
M'Baye Niang
M'Baye Niang, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal, AC Milan na Spurs, sasa anaweza kwenda Everton
Chelsea imeiambia Barcelona kwamba beki David Luiz hauzwi kwa bei yoyote.
Reading ipo kwenye mazungumzo na West Ham juu ya kumnunua mshambuliaji wa Hammers, Carlton Cole kwa pauni Milioni 5.
Mshambuliaji wa Kibrazil, Willian ameomba klabu yake Shakhtar Donetsk isizuie uhamisho wake wa pauni Milioni 20 kwenda Tottenham.
Mchezaji wa Middlesbrough, Marvin Emnes na Tom Ince wa Blackpool wanatakiwa sana na Swansea City.

OBI MIKEL AIPA UBINGWA CHELSEA LIGI KUU

Kiungo wa Chelsea, John Obi Mikel anaamini mbio za ubingwa wa Ligi Kuu zitakuwa ngumu msimu huu lakini amesistizaThe Blues wanaweza kuibuka mabingwa.
Theo Walcott yupo kwenye mazungumzo na Arsenal juu ya mkataba mpya wa miaka mitano kuendeleea kuishi Emirates.
Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez amesema kwamba yupo katika timu nzuri, ingawa ana hasira uwanjani.