|
Gadna akizungumza na Waandishi wa Habari katika mgahawa wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji leo. Wengine kulia kwake ni Scholastica Mazula, Cliffor Ndimbo na Hadija Shaibu 'Dida'. Kulia ni Jabir Saleh. Watangazaji wa Times Radio 100.5. FM |
|
Gadna kushoto akiwa na Schola na mtangazaji mwingoine mpya wa Times, Natasha ambaye anatangaza kipindi cha Filamonata. |
|
William Malacela akimpongeza Gadna |
|
Waandishi wa Habari waliohudhuria utambulisho wa Gadna Times FM leo wakipata maakuli |
MTANGAZAJI
Super Star bongo, Gadna G. Habash leo ametambulishwa rasmi kuhamia Radio Times FM,
baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili, tangu aipige chini Clouds
FM.
Sauti
tamu ya mume huyo wa mwanamuziki nyota Tanzania, Lady Jaydee sasa itakuwa
ikisikika kwenye kipindi cha Maskani, kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa1:00
usiku.
Mara
ya mwisho, Kapteni G alikuwa akitangaza kipindi cha Jahazi Clouds kabla ya kubwaga
manyanga Novemba mwaka 2010 katika kipindi ambacho redio hiyo ilipoteza mastaa
wengi, wakiwemo Fina Mango, George Njogopa na Masoud Kipanya.
Fina
kwa sasa yupo Magic FM na Kipanya alimtangulia Gadna Times. Kwa sasa, bila
kutafuna maneno, Times FM ipo juu ‘kinoma’ katika FM radio za kibongo na
nyingine nyingi zimebakiza umaarufu wa majina tu.
|
Mona na mama yake, watangazaji wa Filamonata Times FM |
|
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto katikati, kulia Mkurugenzi wa Jambo Concept Inc, Benny Kisaka na William Malecela, walikuwepo kwenye utambulisho huo |
|
Willy Malecela akiwa na vifaa vya Times FM |
0 comments:
Post a Comment