NYOTA wa mpira wa kikapu kutoka Marekani, Hasheem Thabeet Mtanzania
anayehezea Oklahoma City, Luol Deng Muingereza mwenye asili ya Sudan Kusini, anayechezea
Chicago Bulls leo wameendesha programu ya kliniki kusaka vipaji vya mpira wa kikapu
kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es Salaam kwenye viwanja vyta Don
Bosco, Upanga.
Kliniki hiyo ilihudhuria na nyota wengine wa NBA, akiwemo Adam
Andre, Masai Ujiri, mmiliiki na Meneja wa timu ya Denver Nuggets, Amadaou Gall
Fall na Kocha J.
Alikuwepo pia Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo Tanzania,
Juliana Yassoda, Balozi Mdogo wa Marekani, Robert K Scott, Rais wa Chama
cha Mpira wa Kikapu (TBF), Mussa Mziya na
Makamu wake, Phares Magesa.
Zoezi
lilianza saa nne asubuhi kwa hotuba ndefu, zilizowafanya watoto waungue juwa
muda wa zaidi ya saa mbili, kabla ya kuanza kupewa mafunzo hayo. Pichani ni watoto waliohudhuria wakiteseka na jua kwa kusikiliaza hotuba ndefu. |
0 comments:
Post a Comment