Ali Mafuruki |
Na Princess Asia
Wanachama wa klabu ya Gymkhana juzi walimuondoa
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ali Mafuruki na viongozi wenzake na kuundwa kamati ya
muda inayokaa madarakani hadi Septemba mwaka huu.
Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano uliopo ndani ya viwanja Gymkhana Dar es Salaam, walifikia uamuzi wa
kumuondoa Mafuruki kwa kuiendesha klabu hiyo kibabe na kuondoa taratibu nyingi
ambazo zimekuwa kero kwa wanachama.
Hali iliyomfanya mmoja wa wanachama wa klabu hiyo,
ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), hasiwe mbiashi
kujiondoa kwani hasifanye Gymkhana kama Woorlworth ambayo ni moja ya kampuni
anazomiliki Mafuruki.
Kufuatia uamuzi huo, wanachama hao wameteua kamati ya
muda itayayoongozwa na Victor Kimesera na Makamu wake Erard Mutalemwa, huku manahodha wa michezo yote wanendelea na
nyadhifa zao ambao ndio wanaounda kamati ya utendaji ya Ghymkhana.
Mkutano huo ulianza saa moja na nusu juzi usiku huku
kukiwa na polisi waliokuwa na lengo la kulinda usalama, lakini ulitawaliwa na
jazba ya kumtaka Mafuruki ajiuzuru kwa madai kuiendesha klabu hiyo kinyume na
taratibu na maamuzi mengi yamekuwa yake binafsi.
Hata hivyo, Mafuruki baada ya kuingia katika mkutano
huo aliwaambia wanachama hao kuwa mkutano huo haukufuata taratibu hivyo maamuzi
yoyote ambayo watayachukua yatakuwa yamekiuka katiba ya klabu hiyo na kususia
kikao na kuondoka.
Wakati akiondoka wanachama hao walikuwa wakizome,
hali iliyofanya mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo Jaji mstaafu, Stella Longway
kuchukua jukumu la kuendesha kikao kwa mujibu wa katiba yakbu hiyo na wanachama
kufukia maamuzi ya kuwaondoa viongozi wote wa klabu hiyo.
Klabu hiyo mbali na Jaji Stella inawadhani wengine
wawili ambao ni G. Kilindu na Ritha Akena.Wadhamini hao wana mamlaka ya kufanya
kazi hiyo kwa niaba ya wanachama wa klabu hiyo.
Kufuatia uamuzi huo, kamati hiyo ya muda inayoongozwa
na Kimesera inatarajia kukutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ni
kurudisha ada ya mgeni mwalikwa ‘Guest Fees” kutoka shilingi elfu 10 hadi elfu
mbili kama zamani.
Hatua nyingine ni kurudisha utaratibu wa timu za
Gymkhana kualika timu za nje kucheza mechi, hali ambayo uongozi wa Mafuruki
ulipiga mafuruku kucheza mechi ndani ya viwanja hivyo au timu zinazokuja
kulipiwa shilingi elfu 10 kwa kila mchezaji.
Mbali na Mafuruki kama Mwenyekiti, wengingine ni
Makamu Mwenyekiti, Profesa Primo Carneiro,Katibu Nicholas Siwingwa, Mweka
hazina, Nada Margwe, Mkuu wa wanachama, Santosh Gajjar, Mkuu wa viwanja, David
Shambwe, Mkuu wa Bar, Alfred kinshwaga na Joseph Kusaga mkuu wa kitengo cha
burudani.
Wengine ni manahodha michezo yao kwenye mabano ni
Joseph Tango (Gofu),Inger Njiru (Tenisi),Chukkapalli Sriram (Kriketi),Ivan
Tarimo (soka),Deepak Dosh (squashi) na Firoz Yusufunali (snooka)
Lakini wanachama hao wanakusudia kuwarudia wakuu wa
vtengo vyote kasoro nafasi ya Mwenyekiti.
0 comments:
Post a Comment