Nsajigwa |
Na Princess Asia
NAHODHA wa zamani wa
timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Nsajigwa Shadrack Joel
Mwandemele, ni miongoni mwa wadau wanaotarajiwa kushiriki Kozi ya Uongozi na
Utawala ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) itafanyika katika ukumbi wa Msimbazi
Center, Dar es Salaam kuanzia Agosti 6-11 mwaka huu ikiwa na washiriki 30.
Kwa ujumla, washiriki
wa kozi hiyo itakayonedeshwa na wakufunzi kutoka FIFA ni viongozi kutoka TFF,
Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), vyama vya mpira wa miguu vya mikoa,
klabu za Ligi Kuu na viongozi wa mpira wa miguu wa wanawake.
Walioteuliwa kushiriki
ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani
Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo,
Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.
Wengine ni Katibu Mkuu
wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama
vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro
Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
Makatibu wa vyama vya soka
vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi
Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima).
Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa
Yanga, Clement Sanga.
Washiriki wengine ni
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa
Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe,
Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba, Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay,
Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa
miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.
0 comments:
Post a Comment