VICHWA VINAUMA; Makocha wa Coastal, Juma Mgunda kulia na Msaidizi wake, Habib Kondo kushoto |
Na Princess Asia
COASTAL
Union imefungwa mabao 2-0 jioni hii na Bandari ya Mombassa, Kenya katika mchezo
wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Mabao
ya Bandari inayocheza Ligi Daraja la Kwanza Kenya, yalitiwa kimiani na kiungo
David Naftali dakika ya 27 kwa shuti la umbali la mita 35, baada ya kupewa pasi
na mshambuliaji Thomas Marucie, wote Watanzania.
Bao
la pili lilifungwa na Evan Wandela dakika ya 88 kwa kichwa akiunganisha kona
iliyochongwa na Hussein Puzzo.
Baada
ya mchezo huo, mashabiki wa Coastal waliwatia kashikashi makocha Juma Mgunda na
Msaidizi wake Habib Kondo wakidai hawafai na kutaka waondolewe, hali ambayo
ilifanya waondolewe uwanjani kwa msaada wa Polisi.
Hali hii inajitokeza kwa mara ya pili, baada ya juzi
pia timu hiyo ikicheza na JKT Oljoro ya Arusha pamoja na kushinda bao 1-0, mashabiki
walilalamikia kiwango kibovu na kuzomea makocha. Jumamosi, Coastal itacheza
Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment