Kocha
Mgunda akizungumza na wachezaji
|
Kocha
Mgunda akizungumza na wachezaji
|
Kocha
Mgunda akizungumza na wachezaji
|
Kocha
Mgunda kulia, na Msaidizi wake Kondo
|
Wachezaji
wakimsikiliza kocha wao
|
Viongozi;
kutoka kulia, Mwenyekiti Ally Ahmad Hilal ‘Aurora’, Katibu Kassim El Siagi na
Meneja Akida
|
Kulia
ni Nahodha Said Swedi ‘Panucci’ akiwa na wachezaji wenzake wakimskiliza kocha
|
Mafaza;
Kulia ni Razack Khalfan, nyuma yake Jackson Chove, nyuma kabisa Juma Mpongo na
mbele yake kushoto ni Suleiman Kassim ‘Selembe’
|
Wa
kwanza kulia Aziz Gilla, anayemfuati ni Jerry Santo na mbele yao ni Juma Jabu,
ambao wote walikuwa Simba SC
|
Kushoto
ni Pius Kisambale
|
BAADA
ya jana kuonyesha kiwango duni, wakimenyana na JKT Oljoro ya Arusha pamoja na
kushnda bao 1-0, Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wachezaji wa Coastal Union
leo asubuhi wamewekwa ‘kiti moto’ na makocha wao baada ya mazoezi ya asubuhi,
kwenye Uwanja huo.
Kocha
Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda aliwaleza wazi wachezaji wa timu hiyo matatizo
yao ya kiuchezaji akitolea mfano mechi mbili zilizopita, ya jana dhidi ya
Oljoro na Polisi mjini Morogoro.
Alitumia
takriban saa nzima akizungumza na wachezaji hao, ambao walionekana kutulia
wakimsikiliza kwa makini.
Katika
mchezo wa jana wa kirafiki, kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotarajiwa
kuanza Septemba 15, bao pekee la mabingwa hao wa 1988, lilitiwa kimiani na beki
mpya aliyesajiliwa kutoka Simba SC, Juma Jabu dakika ya 32 baada ya kupanda
mbele kusaidia mashambulizi akiteleza kutokea wingi ya kushoto.
Huo
ni ushindi wa kwanza wa Wagosi hao wa Kaya, ndani ya mechi tatu zsa kujipima
nguvu, ikitoka kufungwa 3-2 na Bandari mjini Mombasa, Kenya na 1-0 dhidi ya
Polisi mjini Morogoro.
Pamoja
na ushindi huo, mashabiki wa Coastal hawakuridhishwa na kiwango cha timu na kuanza
kubeza uwezo wa makocha wa timu hiyo, Juma Mgunda na msaidizi wake, Habib
Kondo.
Habari
za ndani zinasema kwamba Coastal inafikiria kubadilisha benchi la ufundi
kutokana na kutoridhishwa na uwezo wa timu.
Coastal
iliwekeza kwenye usajili wa kishindo, ikiamini itafanya vizuri katika Ligi Kuu,
lakini kwa matokeo haya ya awali tayari hofu imeanza kuingia na wakati
mashabiki wakitilia hofu uwezo wa makocha, wengine wanatilia hofu uwezo wa
wachezaji waliosajiliwa, wakiamini inaweza kuwa ni bora kwa majina tu.
Kikosi
cha Coastal kinaundwa na makipa; Juma Mpongo, Abraham Chove na Rajab Kaumba,
mabeki; Said Sued (Nahodha) Mbwana Kibacha (Nahodha Msaidizi) Othman Omary,
Juma Jabu, Ismail Suma, Jamal Machelenga, Cyprian Lukindo na Philipp Mugenzi.
Viungo watakuwa ni Jerry Santo, Razack Khalfan,
Mohamed Binslum, Khamis Shango, Mohamed Issa, Mohamed Soud, Suleiman Kassim
‘Selembe’, Lameck Dayton, Joseph Mahundi, Aziz Gilla na Shaffih Kaluani, wakati
washambuliaji ni Nsa Job, Atupele Green, Danny Lianga na Pius Kisambale.
Mbali na Kocha Mkuu, mshambuliaji wake wa zamani,
Mgunda, na Msaidizi wake, beki wa zamani
wa Pan African, Habibu Kondo, benchi la ufundi la Coastal linakamilishwa na kocha
wa viungo, mchezaji wake wa zamani, Ally Jangalu na kocha wa makipa Bakari
Shime.
0 comments:
Post a Comment