Chuji |
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars, Mdenmark Kim Poulsen leo ametaja kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya
mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu, ndani yake akiwaita
kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na mfungaji bora wa Klabu Bingwa ya Soka Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame, Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Hata hivyo, ajabu Poulsen amemuacha kikosini kipa Ally Mustafa
Mtinge ‘Barthez’ aliyedaka kwa umahiri mkubwa, mechi tatu za Kagame, Robo
Fainali, Nusu Fainali na Fainali, hadi kuiwezesha Yanga kutwaa taji, huku
akimuita kipa Mwadini Ally wa Azam, ambaye hajadaka hata mechi moja kwenye
mashindano hayo.
Bahanuz |
Makipa walioitwa kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi
(Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha
msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na
Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna
Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo
(Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi
(Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samatta (TP
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon
Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
DRC).
0 comments:
Post a Comment