David Naftali |
Na Princess Asia
BANDARI ya Mombasa,
Kenya inayopigwa tafu na wachezaji wanne wa Kitanzania, David Naftali, Meshack
Abel, Mohamed Banka na Thomas Maurice, imeendelea kujiimarisha katika harakati
za kurejea Ligi Kuu ya Kenya, baada ya jana kuifunga mabao 2-0 Moyas ya Nairobi.
Bandari ilipata bao
lake la kwanza dakika ya tano, mfungaji Thom Mouricekwa mpira wa adhabu, kabla
ya Erick Okoth kufunga la pili dakika ya 38.
Kwa ushindi huo, Bandari
imefikisha pointi 60, ikizidi kuwaacha mbali wapinzani wao, Kariobang Sharks
wenye pointi 49 katika nafasi ya pili, baada ya kutoka sare na Kongo United (JMJ)
jana.
Bandari inatarajiwa kuondoka
Mombasa kesho kuja Dar es Salaam kwa ziara ya wiki moja ya kucheza mechi za
kujipima nguvu.
0 comments:
Post a Comment