Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya
ANCELOTTI AIBOMOA CHELSEA
KOCHA Carlo Ancelotti anataka kuungana tena Ashley Cole na anataka kumsajili beki huyo wa Chelsea katika klabu yake mpya, Paris Saint-Germain.
Arsenal inataka kumsajili kiungo mkabaji Mkenya wa Celtic ya Scotland, Victor Wanyama, mwenye umri wa miaka 21, kama mbadala wa Mcameroon Alex Song, ikiwa atahami Barcelona, ambao wanamtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.
Juventus imempa muda Robin van Persie kuweka fikra zake katika kuhamia Italia, na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, bado anataka kuondoka Arsenal.
Real Madrid inandaa dau la pauni Milioni 19.7 kwa ajili ya kumsajili winga wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25.
Santi Cazorla, mwenye umri wa miaka 27, amekwenda kufanyiwa vipimo vya afya Arsenal na klabu hiyo inatarajiwa kutangaza kumnunua kwa dau la pauni Milioni 16 kutoka Malaga.
Manchester City imeonyesha nia ya kumsajili beki mwenye umri wa miaka 22 wa Marseille, Nicolas N'Koulou.
MUAMBA KUANZA MAZOEZI
BEKI wa Bolton, Fabrice Muamba, mwenye umri wa miaka 24, atasafiri hadi Ubelgiji wiki ijayo kwenda kumuona mtaalamu ili kujua mustakabali wake wa kurejea mazoezini.
KIUNGO wa zamani wa Fulham na Tottenham, Steed Malbranque, mwenye umri wa miaka 32, anajiandaa kurejea kwenye soka ya kulipwa baada ya muda usiozidi mwaka mmoja tangu atangaze kustaafu.
POMPEY WAPAMBANA NA DHIKI
Portsmouth inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya AFC Wimbledon wiki ijayo katika jitihada za kupambana na hali ngumu ya kifedha inayowakabili kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment