Klabu ya Yanga imepongezwa kwa juhudi mbalimbali katika kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini pamoja na harakati za uhuru wa Tanzania na Msumbiji.
Wakizungumza wakati wa ziara yao wakati walipotembelea Makao Makuu ya Klabu ya Yanga Kiongozi wa msafara huo Florinda Mauribe kutoka Chuo cha Ualimu cha Ajuda do Dusenvolinmento do Povopara O Povo-Escola de Professones do Futuro-Chimdio, alisema wamejisikia furaha sana kufika makao makuu ya klabu ya Yanga, kuona mazingira ya klabu na kupewa historia fupi ya timu hii kongwe katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Mauribe amesema Wananchi wa Msumbiji wanathamini mchango mkubwa wa ukombozi wa nchi yao kwa Tanzania ikiwemo Yanga ambapo wananchi hao wanayo taarifa kuwa baadhi ya Wapenzi na Mashabiki wa Yanga walitoa mchango wa hali na mali katika kusaidia harakati za ukombozi katika nchi hiyo ya Msumbiji.
Wanafunzi hao walitembezwa katika jengo la Makao Makuu ya Klabu ya Yanga na kujionea mambo mbalimbali ikiwemo Uwanja wa Kaunda unaotarajiwa kufanyiwa matengenezo,Gym ya mazoezi,Bwawa la kuogelea na Mtandao wa Klabu ya Yanga wa www.youngafricans.co.tz.
0 comments:
Post a Comment