Kikosi cha kwanza cha Yanga, ambacho kinaendelea na mazoezi Dar es Salaam, wakati wadogo zao wapo visiwani Zanzibar |
Na Prince Akbar
MICHUANO ya Kombe la Urafiki, inatarajiwa kuendelea leo
kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa Yanga kumenyana na Jamhuri ya Pemba.
Yanga ambayo imepeleka wachezaji wake wa kikosi cha vijana
visiwani humo, imeahidi kuongeza wachezaji kulingana na maendeleo ya timu.
Katika mechi za ufunguzi jana, Simba SC walianza vyema baada
ya kuwafunga wenyeji Mafunzo mabao 2-1, wakati Azam ililazimishwa sare ya 1-1
na U23, Karume Boys.
Abdallah Juma, ambaye amepokewa Simba kama Emmanuel Gabriel
mpya, alifunga bao la kwanza dakika ya 27 akiunganisha pasi muruwa ya Patrick
Kanu Mbivayanga dakika ya 27.
Mshambuliaji huyo mrefu kutoka Ruvu Shooting ya Pwani, alifunga
bao la pili dakika ya 44 kwa kichwa, akiunganisha pasi ya Mbiyavanga tena,
kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mafunzo walipata bao lao dakika ya 80, mfungaji Jaku Joma.
Katika mchezo wa leo, kwa mara ya kwanza mshambuliaji Danny
Mrwanda aliichezea Simba tangu asajiliwe tena mwezi uliopita akitokea Dong Tam
Long An ya Vietnam.
Simba, mabingwa wa Tanzania walichezesha kikosi chao kamili,
ingawa Emmanuel Okwi, Felix Sunzu na Haruna Moshi ‘Boban’ wameendelea
kukosekana.
Simba; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah/Paul Ngalema,
Lino Masombo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Danny Mrwanda/Mwinyi Kazimoto,
Mussa Mudde/Paul Ngalema, Abdallah Juma/Uhuru Suleiman, Kanu Mbivayanga/Haroun
Othman na Kiggi Makassy.
Mafunzo: Suleiman Janabi, Hajji Abdi, Ally Juma, Yussuf
Makame, Said Mussa, Juma Othman, Abdulrahim Mohamed, Suleiman Kassim ‘Selembe’,
Ismail Khamis, Juma Jaku na Ally Othman.
Azam ilinusurika kulala mbele ya timu ya taifa ya vijana
chini ya umri wa miaka 23 (U23) ya Zanzibar, Karume Boys baada ya kulazimisha
sare ya kufungana bao 1-1.
Karume Boys walipata bao la kuongoza dakika ya 45 kwa njia ya
penalti, mfungaji Ibrahim Hamisi.
Kipindi cha pili Azam walikuja juu na dakika ya 79
wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre
Tcheche.
RATIBA KAMILI
MICHUANO YA URAFIKI
Julai 2, 2012
Karume Boys 1-1 Azam
Mafunzo 1-2 Simba SC
Julai 3, 2012
Z’bar Stars Vs Super Falcon
Jamhuri Vs Yanga SC
Julai 4, 2012
Karume Boys Vs Mafunzo
Simba SC Vs Azam
Julai 5,2012
Super Falcon Vs Jamhuri
Yanga Vs Zanzibar Stars
Julai 6, 2012
Azam Vs Mafunzo
Karume Boys Vs Simba SC
Julai 7, 2012
Jamhuri Vs Zanzibar Stars
Super Falcon Vs Yanga SC
Julai 8, 2012
MAPUMZIKO
Julai 9, 2012
Nusu Fainali ya kwanza
Julai 10, 2012
Nusu Fainali ya pili
Julai 11, 2012
MAPUMZIKO
Julai 12, 2012
Fainali
(Mechi za kwanza zitachezwa saa 10:30 jioni na mechi za pili saa 2:00
usiku, Uwanja wa Amaan)
0 comments:
Post a Comment