|
Yanga wakishangilia baada ya kumaliza kazi |
|
Kipa wa Mafunzo, Mahadhi akiokoa mbele ya Bahanuzi |
|
Hatari langoni mwa Mafunzo |
|
Beki wa Mafunzo anamgeuza Kiiza kwenye eneo la hatari na kuokoa |
|
Juma Abdul anajiandaa kutia krosi |
|
Heka heka |
|
Hii ni dua ambayo Mafunzo walisoma baada ya dakika 45 wakiwa wanaongoza 1-0 |
|
Kikosi cha ushindi Yanga |
|
Makocha wa Yanga |
|
Kocha wa Mafunzo; Ahmed Morocco |
|
Chuji |
|
Chuji kulia akikimbia na Barthez baada ya kufunga penalti ya mwisho |
|
Kiiza na Tegete |
|
Yanga wakishangilia |
|
Yanga wakiomba dua |
|
Yanga wakiomba dua kabla ya penalti |
|
Said Bahanuzi chini katika mishemishe za kusaka mabao |
|
Yanga baada ya dakika 90 za 1-1 |
|
Jerry Tegete kulia na Haruna Niyonzima kushoto wakimpongeza Chuji- nyuma nyuma ni Bahanuzi 'Spider Man' |
|
Benchi Yanga likiomba dua wakati Chuji anakwenda kupiga penalti ya mwisho |
|
Said Bahanuzi 'Spider Man'' |
|
Mmanga akiwa kwenye machela baada ya kupoteza fahamu |
|
Hapa ni mara tu baada ya kuanguka akisaidiwa kwa kupepewa na wenzake |
YANGA imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka
Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Mafunzo ya
Zanzibar kwa penalti 5-3, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Wawakilishi wa Zanzibar Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao
lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika ya 34, akiunganisha kona ya Juma
Othman Mmanga na Yanga wakasawazisha dakika ya 46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider
Man’.
Yanga sasa itamenyana na APR ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika
Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake
yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya
34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala, lilifungwa na Robert Ssentongo dakika
ya 57.
Katika mchezo huo, Juma Othman Mmanga alipoteza fahamu na
kuwaweka roho juu wachezaji wenzake na mashabiki, akatolewa nje akipepewa na
hakuweza kuendelea na mchezo, lakini taarifa za baada ya mchezo zilisema anaendelea
vizuri.
Kipa wa Yanga Berko aliumia dakika ya 69 na akatibiwa kwa
dakika tatu, kabla ya kutolewa nje dakika ya 72, nafasi yake ikichukuliwa na
Ally Mustafa Barthez ambaye ukaaji wake mazuri langoni wakati wa penalti ulimfanya
Said Mussa Shaaban wa Mafunzo akapiga nje na kuipa Yanga ushindi.
Saidi Bahanuzi alipiga penalti ya kwanza, Nahodha Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ ya pili, Hamisi Kiiza ya tatu, ya nne Haruna Niyonzima na
Athumani Iddi ‘Chuji’ alipiga ya mwisho na kuwainua maelfu ya mashabiki wa
Yanga Uwanja wa Taifa.
Yanga SC; Yaw
Berko/Ally Mustafa, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin
Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika/Idrissa Assenga, Haruna Niyonzima,
Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo/Jerry Tegete.
Mafunzo; Khalid Mahadhi
Hajji, Ismail Khamis Amour/Hajji Abdi Hassan, Said Mussa Shaaban, Salum Said
Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga/Sadik Habib Rajab, Suleiman Kassim
‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim/Kheir Salum Kheir
na Ally Juma Hassan.
0 comments:
Post a Comment