Green kulia katika mechi ya jana |
Na Prince Akbar
MWAKA 2010, Atupele Green aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa
akademi au timu ya vijana kusajiliwa kwa bei mbaya zaidi katika soka ya
Tanzania, baada ya kusajiliwa na Yanga kwa Sh. Milioni 27, enzi hizo Katibu
Mkuu, Lawrence Mwalusako na Kocha Mkuu Kosatadin Papic, Meneja Emmanuel
Mpangala.
Lakini tangu asajiliwe, Green hajawahi kuchezea kikosi cha
wakubwa cha Yanga na sasa inaelezwa mchezaji huyo amesajiliwa Coastal Union ya
Tanga, kama mchezaji huru, kwa kuwa amekwishamaliza makataba wake Jangwani.
Kwa sasa Green, ndiye mshambuliaji tegemeo wa timu ya soka
ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes ambayo jana ilifungwa
mabao 2-1 nyumbani na Nigeria katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali
za Mataifa ya Afrika kwa vijana.
Achaji Gero wa Enugu Rangers, wapinzani wa zamani wa Yanga,
ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Flying Eagles, wakati Green alifunga bao
la kufutia machozi la Ngorongoro.
Wakati Yanga ikimuacha Green akienda Coastal, yenyewe
imevunja benki yake na kusajili wachezaji wawili wa Ngorongoro, kiungo Frank
Damayo na mshambuliaji wa pili, Simon Msuva.
Katika Ngorongoro ya sasa, Green na Msuva wanacheza kama
washambuliaji pacha, wakicheza kwa uelewano mkubwa na kiungo mshambujliaji, Ramadhani
Singano ‘Messi’.
0 comments:
Post a Comment