Wachezaji wa Yanga; Picha hii ni haki miliki ya BIN ZUBEIRY. Aliipiga katika mechi na Express ya Uganda, mchezo wa kirafiki wiki mbili zilizopita. |
Na Prince Akbar
MABINGWA watetezi wa Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki
na Kati, Yanga SC ya Dar es Salaam, leo wanatarajiwa kutupa karata yao ya pili
katika michuano hiyo, watakapomenyana na Waw Salaam ya Sudan Kusini, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inahitaji ushindi katika mchezo wa leo, ili kurejesha
imani kwa mashabiki wake, baada ya kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza na
Atletico ya Burundi.
Waw Salaam inaonekana kuwa dhaifu, kwani katika mchezo wa
kwanza ilitandikwa na APR ya Rwanda mabao 7-0, hivyo kwa Yanga leo inaweza siku
nzuri ya kujipima na kupata taswira nzima ya ushiriki wao katika mashindano
haya.
Katika mchezo wa leo, Yanga iko hatarini kuwakosa wachezaji
wake watatu nyota, kipa Ally Mustafa Barthez, beki wa kulia Juma Abdul na
kiungo Haruna Niyonzima kwa sababu ni majeruhi.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet aliiambia BIN
ZUBEIRY jana kwamba anasikitika mno alipanga kumuanzisha Barthez katika
mechi ya leo, lakini kwa kuwa ameumia sasa atalazimika kuanza na Mghana Yaw
Berko tena aliyetunguliwa mawili, Yanga ikilala 2-0 mbele ya Atletico FC ya
Burundi juzi.
Kwa kuumia wachezaji hao, sasa Yanga inabakiwa
na wachezaji 17 walio fiti, ambao ni kipa;
Yaw Berko, mabeki;, David
Luhende, Kelvin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Godfrey Taita, Ladislaus
Mbogo, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika, viungo;
Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Shamte Ally, Nizar
Khalfan na Idrisa Assenga na washambuliaji;
Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Jerry Tegete.Mechi ya leo itatanguliwa na mechi kati ya APR ya Rwanda na Atletico ya Burundi, mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Mabingwa wa Tanzania, Simba waliolanza kwa kufungwa 2-0 na URA ya Uganda juzi, watacheza tena kesho dhidi ya Ports ya Djibouti
iliyofungwa 7-0 na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika
mchezo wa kwanza, mechi ambayo itatanguliwa na mchezo kati ya Vita Club na URA
ya Uganda.
Wamiliki wa Medali ya Fedha ya Ligi Kuu, Azam FC walioanza kwa sare ya 1-1 na Mafunzo ya Zanzibar watarejea uwanjani Julai 21, kumenyana na Tusker FC ya
Kenya .
0 comments:
Post a Comment