Atletico FC itakayofungua dimba na Yanga |
Na Princess Asia
KLABU za El Salam Wau ya Sudan
Kusini na Atletico ya Burundi zinatarajiwa kuwa timu za kwanza kuwasili nchini
kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
Michuano hiyo inaanza kutimua
vumbi Jumamosi (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
ikishirikisha timu kumi na moja akiwemo bingwa mtetezi Yanga na makamu bingwa
Simba.
Ofisa Habari wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY mchana wa leo
kwamba, kikosi cha El Salam Wau ambacho kitawasili kesho alfajiri (Julai 11
mwaka huu) kwa ndege ya Ethiopia Airlines kikitokea Juba kupitia Addis Ababa,
Ethiopia kikiwa na wachezaji 18 na viongozi saba.
Amewataja wachezaji wanaounda
kikosi hicho ni Khamis Leone Uso Wani (nahodha), Adheil Bugwic Jongkor Bugwic,
Edward Joram Simon Julio, Fidel Andrea Fides Fas, Ismael Musa Juma Ismael,
James Anei Matheli Anei, Jervas Ayo Abdalla Ayak, Khamis Doshama Ulama Andel na
Meki Sultan Berema Kuku.
Amewataja wengine ni Moga
Emmanuel Androga, Mubarak Mohammed Saleh Omer, Ndili Rabeh Nasir Hozi, Nizir
Rihan Taban Talib, Oliver Paul Kangi Akok, Rabie Mohammed Abubakar Hassan,
Rufino Joseph Uras Ambros, Santino Makuei Uyu Upio, Thomas Rufino Thomas
Diakon.
Amesema Atletico nao wanatarajiwa
kuwasili kesho (Julai 11 mwaka huu) kwa usafiri wa barabara. Timu hiyo inakuja
kwa usafiri wa basi lake ambalo pia italitumia kwa muda wote itakapokuwa kwenye
mashindano.
Amesema wakati El Salam Wau
itafikia kwenye hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya Kariakoo, Atletico itakuwa
Lunch Time Hotel iliyoko Mabibo.
Amezitaja timu zinazotarajiwa
kuwasili keshokutwa (Julai 12 mwaka huu) ni Mafunzo ya Zanzibar kwa boti saa 9
alasiri, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) itatua saa 1.20
usiku kwa Kenya Airways. Timu nyingine itakayowasili siku hiyo jioni ni URA ya
Uganda.
0 comments:
Post a Comment