Thomas Ulimwengu wa Ngorongoro |
Na Prince Akbar
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka
Kenya kuchezesha mechi ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro
Heroes) na Nigeria.
Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya
pili itakayofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
atakuwa Moses Ojwang Osano.
Waamuzi wasaidizi watakuwa Peter Keireini na Elias Kuloba
Wamalwa wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Thomas Onyango. Kamishna
wa mechi hiyo atakuwa Charles Masembe kutoka Uganda.
Pia CAF imemteua Alfred Kishongole Rwiza wa Tanzania kuwa
Kamishna wa mechi ya michuano hiyo kati ya Misri na Kenya itakayochezwa jijini
Cairo kati ya Julai 27, 28 na 29 mwaka huu
0 comments:
Post a Comment