Tetesi za J'pili magazeti ya Ulaya

VAN PERSIE KWENDA NA ARSENAL BEIJING

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Robin van Persie anatarajiwa kujumuika kwenya kikosi cha timu yake katika ziara ya kujiandaa na msimu mpya bara la Asia, Beijing Jumamosi ijayo, iwapo Manchester City, au Juventus hawatafanikiwa kukamilisha uhamisho wake mapema.
KLABU ya Ajax inafikiriwa kuwa katika mazungumzo na klabu mbili juu ya mchezeshaji wa kimataifa wa Denmark, Christian Eriksen, ambaye anatakiwa na Manchester United na Barcelona.
TAARIFA kutoka Ufaransa zinasema kwamba Laurent Koscielny, ambaye inaaminika ameanza mazungumzo ya mkataba mpya na Arsenal, anatakiwa na Barcelona.
KOCHA mpya wa Newcastle, Alan Pardew amesema kwamba klabu hiyo inaweza kusaini wachezaji wawili au watatu wapya bila kuhitaji kuuza hata mchezaji mmoja kwenye kikosi chake cha sasa.

AVB AWAKANDIA CHELSEA NA ABRAMOVICH

KOCHA mpya wa Tottenham, Andre Villas-Boas ameipiga madongo klabu yake ya zamani, Chelsea na mmiliki wake, Roman Abramovich huku akimwagia sifa Mwenyekiti mpya, Daniel Levy.
MCHEZAJI mpya wa Arsenal, Lukas Podolski amemtaka mshambuliaji Robin van Persie, ambaye amesema hatasaini mkataba mpya wakati huu wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu ujao, kubaki katika klabu hiyo.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Everton, Graeme Sharp amesema mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Michael Owen anaweza kutua Goodison Park.

BALOTELLI NDIYE SHUJAA WA TEVEZ...

BAADA ya kuulizwa na shabiki ni yupi mchezaji wake anayemvutia na shujaa wake, mshambuliaji wa Manchester City, Carlos Tevez alijibu ni Mario Balotelli.