Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya

JUVE YAZIPIGA BAO MAN CITY, MAN UNITED SAINI YA VAN PERSIE

KLABU bingwa ya Italia, Juventus iko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, baada ya kuzizidi kasi Manchester zote, United na City.
KLABU ya Tottenham iko tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya Rafael van der Vaart, mwenye umri wa miaka 29. Ada ya uhamisho ya pauni Milioni 10 na ushei zinaweza kutosha kumnyakua kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi.
KLABU ya Tottenham inapiga mishemishe za kumrejesha katika Ligi Kuu ya England kiungo wa zamani wa Chelsea, Arsenal na Portsmouth, Lassana Diarra, mwenye umri wa miaka 27, baada ya kuambiwa anaweza kuondoka Real Madrid.
Bridge spent five months on loan at Sunderland
KLABU ya Brighton inataka kumchukua kwa mkopo beki wa Manchester City, Wayne Bridge msimu ujao. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 31, mwishoni mwa msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Sunderland.
KOCHA wa Tottenham, Andre Villas-Boas ameingia kwenye vita na Sir Alex Ferguson wa Manchester United kwa sababu ya beki Ezekiel Fryers, mwenye umri wa miaka 19, ambaye anajiandaa kusaini Spurs.

SHEVCHENKO KUREJEA CHELSEA

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Andriy Shevchenko, mwenye umri wa miaka 35, anajiandaa kurejea Chelsea kufanya kazi chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich, kwa mujibu wa klabu yake, Dynamo Kiev.