Ramadhani Haruna Shamte |
Na Princess Asia
KLABU ya URA ya Uganda inataka kusajili wachezaji wawili
kutoka Simba, mmoja imesema itatamtaja baadaye, lakini ambaye imeshindwa
kujizuia kabisa ni beki Ramadhani Haruna Shamte.
BIN ZUBEIRY inafahamu URA leo wamefanya mazungumzo na Simba SC
juu ya kusajili wachezaji wawili wa mabingwa hao wa Tanzania, lakini wakasema
mmoja wanahitaji kuendelea kumfuatilia, ila ambaye wamejiridhisha atawafaa ni
beki wa kulia, Haruna Shamte.
Shamte ambaye aliwahi kucheza hadi timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars amerejea Simba msimu huu, baada ya msimu uliopita
kutolewa kwa mkopo Villa Squad iliyoshuka daraja.
Beki huyo, aliyepitia kipindi kigumu msimu uliopita, kuanzia
kutemwa kwa sababu tu ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi ya Kombe la
Shirikisho dhidi ya Daring Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
siri ya mafanikio yake ni kutokata tamaa, kujituma na nidhamu.
Kocha wa Villa, Habib Kondo alimsifia Haruna kwamba ni
mchezaji mwenye nidhamu na bidii ya mazoezi na akamtabiria mafanikio- na sasa
hizi ndizo dalili za mafanikio.
Kwa sasa, kwa Afrika Mashariki na Kati, URA, inayomilikiwa na
Mamlaka ya Mapato Uganda, ni moja ya timu zinazolipa vizuri wachezaji wake na
zisizoendeshwa kwa ubabaishaji.
0 comments:
Post a Comment