Simba SC |
Na Prince Akbar
RASMI Simba SC imetinga Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya URA ya Uganda kuifunga Ports ya
Djibouti, mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ports sasa imeaga na Simba imekuwa moja ya timu tatu
zilizoingia Robo Fainali kutoka Kundi hilo na itaingia kwenye mchezo wa kesho
dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutafuta kupanda
kutoka kutoka nafasi ya tatu ilipo sasa.
Mabao ya URA katika mchezo wa leo, yalitiwa kimiaini na Augustine
Nsumba dakika ya 23, Sam Mubiru dakika ya 38 na Robert Ssentongo dakika ya 56,
wakati la kufutia machozi la Ports lilifungwa na Roland Ayuk Agbor dakika ya 68.
Kwa matokeo hayo, URA inaendelea kuongoza Kundi A, kwa
pointi zake tisa, baada ya kushinda mechi zake zote tatu na AS Vita inashika
nafasi ya pili, wakati
mabingwa wa Tanzania, Simba SC wanashika nafasi ya tatu, kwa
pointi zao tatu baada ya kucheza mechi mbili, kufungwa moja na kushinda moja.
Kazi ngumu iko Kundi B, baada ya jana Tusker ya Kenya,
kutoka sare ya bila kufungana na Mafunzo ya Zanzibar.
Sasa kundi hilo, ambalo kuna Azam FC pia limezidi kuwa gumu
na kesho Tusker na Azam FC zitakamilisha mechi za kundi hilo Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, katika mchezo ambao timu itakayoshinda moja kwa moja itaungana
na Mafunzo kutinga Robo Fainali.
Hatima ya Mafunzo kucheza au kutocheza Robo Fainali
inashikiliwa na mechi hiyo, kwani iwapo timu hizo zitatoka sare ya kuanzia
mabao 2-2 zitakwenda zote Nane Bora na wawakilishi wa Zanzibar watarejea
nyumbani.
0 comments:
Post a Comment