Na Princess Asia
WAKATI Uchaguzi Mkuu wa Yanga utafanyika katika ukumbi wa
Diamond Jubilee, Upanga mjini Dar es Salaam Julai 15, mwaka huu wagombea saba
wako hatarini kuenguliwa.
Hao ni Mgombea Uenyekiti, Sara Ramadham na Ujumbe Ramadhan Mzimba
‘Kampira’, Edgar Fongo, Abdallah Mbaraka, Mohamed Mbaraka, Ahmad Waziri Gao na Shaaban Katwila.
Kwa nini? Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu ameiambia BIN
ZUBEIRY kwamba, Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
imeagiza wagombea hao wawasilishe vyeti vyao halisi mbele ya Kamati ya Uchaguzi
ya Yanga.
“Wanatakiwa hadi Julai 4 wawasilishe vyeti halisi saa 10:00
jioni, na ili kuwapa nafasi hawa kuwasilisha vyeti vyao, muda wa kuanza kampeni
sasa umesogezwa mbele hadi Julai 6,”alisema Sendeu, ambaye amedokeza pia kocha
mpya wa klabu hiyo, Mbelgiji Thom Saintfiet atawasili kesho.
0 comments:
Post a Comment