Wadau wa Tukuyu Stars, kulia Moses Mkandawile, kushoto Godwin Aswile. Wengine wanaotazama kamera ni Kenny Mwaisabula, Richard Mwaikenda na Nsangalufu Joseph |
Niko na jembe, beki 4 wa enzi hizo Yanga, Godwin Aswile Mulimba 'Scania' |
Huge na brother Aswile |
Napiga stori na Moses Mkandawile, kipa wa zamani wa Simba SC |
Aswile na Mkandawile wakinisikiliza kwa makini nikiwakumbusha vitu vyao enzi zao wanacheza soka |
TUKUYU STARS FAMILY
P.O.BOX 61989
DAR ES SALAAM
05/JULY/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
NIA NA MKAKATI WA
KUIFUFUA NA KUIREJESHA TUKUYU STARS
(BANYAMBALA) LIGI KUU TANZANIA BARA
Tukuyu stars ni timu pekee yenye
historia ya aina yake nchini Tanzania. Ilipanda daraja mwaka 1985, ikachukua ubingwa mwaka 1986, ikashuka daraja mwaka
1987, ikapanda tena daraja mwaka 1988 na baada ya misimu kadhaa ikashuka daraja
na kupotea katika ramani ya mpira nchini.
Hii ni historia ya pekee , lakini cha kukumbukwa zaidi ilikuwa ni uwezo
wa kusakata soka la nguvu, kasi, akili na ubunifu wa wachezaji chini ya mwalimu Athuman Juma ( marehemu).
Kutokana na mwenendo na uwezo wa
Tukuyu stars, timu hii ilivuta mashabiki wengi kila kona ya nchi na Duniani. Hivyo wadau, wapenzi na watu
wengine walioguswa na kupotea kwa Tukuyu stars kwenye ramani ya soka nchini
wameanzisha mkakati wa kuifufua na kuirejesha Tukuyu stars kwenye ramani ili
tuendelee kupata ladha tuliyoikosa, yaani zile burudani za akina Selemani Mathew,
Karabi Mrisho, Stephen Mussa ( marehemu), Salum Kabunda Ninja (marehemu), Ally
Kimwaga, John Alex, Richard Lumumba, Aston Pardon na wengineo. Hivyo lengo ni
kuifufua na kurekebisha mfumo wa uendeshaji wa timu uwe wa kisasa hasa kampuni ili
iwe endelevu, shindani na inayojitegemea kiuchumi na kimaamuzi. Kwa maana hiyo
wadau, wapenzi na wengine wote wanaoguswa na kutokuwepo kwa Tukuyu stars
mnaalikwa kujumuika kwenye mpango huu.
Katika kufikia malengo yaliyowekwa
wadau wameanza utekelezaji wa mpango huu katika ngazi mbalimbali ikihusisha wadau
waliopo Dar es salaam na wale waliopo Mbeya.
i)
Vikao
vya wadau waishio Dar es salaam vimeanza na vinaendelea kila ijumaa kuanzia saa
kumi na nusu jioni Kinondoni Mkwajuni, Katumba bar. Mada kuu ikiwa ni namna
bora ya kuifufua na kuirejesha Tukuyu stars.
ii)
Wadau
wa Tukuyu stars waliopo Mbeya wanaendelea na vikao vya kufanikisha siku rasmi
ya kongamano la kufufuka kwa Tukuyu stars.
iii)
Ili
kuleta hamasa na kuibua vipaji vitakavyounda Tukuyu stars ijayo ligi ndogo
imeanzishwa Wilayani Rungwe mahali ilipozaliwa timu hii. Ligi hii inategemea
kukamilika yaani Fainali zake kuwa tarehe 04/08/2012
Siku ya fainali yaani tarehe 04/08/2012
inatarajiwa kuwa siku ya kujadili na
kufufuka rasmi kwa Tukuyu stars, hii ni siku muhimu na inatarajiwa kuwa na
matukio mengi na ya kusisimua. Kutakuwa
na michezo mitatu ya utangulizi kabla ya mchezo wa fainali, pia kutakuwa na
ngoma za asili maarufu kama Ing’oma.
Michezo itakuwa kama ifuatavyo:-
i)
Mechi
ya awali ya vijana chini ya miaka 14 ( under 14) walioalikwa wakishindana na
wenyeji
ii)
Mechi
ya vijana chini ya miaka 17 ( under 17) itafuatia, pia ikihusisha timu waalikwa
watakaoshindana na wenyeji.
iii)
Baada
ya mechi hizo zitafuatia ngoma za asili
(Mang’oma)
iv)
Itafuatia
mechi ya kukata na shoka ya wakongwe (veterans )waliochezea Tukuyu stars na timu
zingine waliopo Dar es salaam chini ya mwalimu Kennedy Mwaisabula ‘’mzazi’’ wakishindana na wakongwe wenzao (veterans)
waliopo Mbeya wakiongozwa na Jimmy Mored na Alex Mwambipile
v)
Baada
ya mechi ya Veterans itafuatia fainali ya ligi inayoendelea, ili kumpata bingwa
wa mashindano yaliyoanza June.
Kilele cha shughuli hii kitahitimishwa
kwa kongamano kubwa la kuifufua rasmi Tukuyu stars, mjadala huu utahusisha
kuona namna bora ya kuendesha timu, na kama ni kampuni basi uuzaji wa hisa
utaanza siku hiyo kwa kuorodhesha majina ya wote wanaopenda kununua hisa za
kampuni na kujadili namna ya upatikanaji wa Bodi ya timu na watendaji wa timu.
Katika kongamano hili zitatolewa tuzo rasmi kwa waanzilishi na viongozi wa
Tukuyu stars, wanaotegemewa kupewa tuzo ni kama Ramnik Patel Kaka (muasisi),
mzee Kasyupa (katibu mkuu wa kwanza), mzee Malakasuka, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Major General (mstaafu) Rashid
Nalihinga Makame , mzee Mwakasala na wale wote waliojitoa kwa hali na mali
kuifanya Tukuyu stars ing’are katika medani ya soka.
Pia vitakabidhiwa vifaa vya awali kwa ajili ya kuanza rasmi
kambi ya timu ya Tukuyu stars.
Maandalizi ya timu ya veterans waliopo
Dar es salaam yanatarajia kuanza siku ya jumamosi na kusimamiwa na mwalimu
Kennedy Mwaisabula katika viwanja vya Harbours Pub kurasini kuanzia saa mbili
asubuhi. Wachezaji wanaotarajiwa kucheza
mechi hiyo na kuanza mazoezi ni:-
i.
Godwin
Aswile ‘’Mlimba’’ ‘’Scania’’ ( Baba
Subi).
ii.
Seleman
Mathew
iii.
Karabi
Mrisho
iv.
Salum
Kussi
v.
Asanga
Aswile
vi.
Mbwana Makata
vii.
Peter
Mwakibibi
viii. Sekilojo Chambua
ix.
Nsajigwa
Mwaisaka
x.
Geofrey
Amanyisye
xi.
Ezekiel
( Masatu)
xii.
Shedrack
Nsajigwa Fusso
xiii. Christopher Michael
xiv.
Lawrence
Mwalusako
xv.
John
Mwansasu
xvi.
Deo
Philip Masanja
xvii. Michael Mbaruku
xviii. Ally Kassimu
xix.
Nsangalufu
Joseph
Kupitia
taarifa hii tunawaalika wachezaji na wadau wote wanaopenda kushiriki kwenye mazoezi na kucheza mechi hii wafike jumamosi asubuhi saa mbili katika viwanja vya Harbours pub.
Vikao vya mikakati ya kufufua Tukuyu
stars vinaendelea kila ijumaa saa kumi na nusu jioni kinondoni Mkwajuni Katumba
bar hivyo wapenzi na wadau wote
mnaalikwa ili tuweze kupanga kwa pamoja, pia tujadili namna ya kusafiri kwenda
Tukuyu Mbeya kwa ajili ya hiyo siku rasmi.
Michezo inaburudisha, inatoa ajira,
inajenga undugu na zaidi ya hapo inawafanya wanajamii wasahau tofauti zao na
kuungana kusonga mbele katika maendeleo yao. Tunawaombeni wadau wote wenye
mapenzi mema na Tukuyu stars tuungane ili turudishe heshima ya miaka ya
1980 wakati Tukuyu stars ikipambana na Simba
ya Dsm, Yanga ya Dsm, Pamba ya Mwanza, Ushirika ya Moshi, Mecco ya Mbeya, Coastal
Union ya Tanga, Nyota Nyekundu ya Dsm, Sigara ya Dsm, Pilsner ya Dsm, Lipuli ya
Iringa na timu nyingine. Tujumuike ili tuzalishe wachezaji mahiri kama Justin
Nicodemus Mtekele ( marehemu), Aston Pardon, Sekilojo Chambua, Hussein Zito,
Stephen Mussa ( marehemu), Jabir Mohamed (
marehemu), Peter Mwakibibi na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment