|
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU UCHAGUZI WA KUJAZA
NAFASI ZA UONGOZI WA KLABU YA YANGA
10 JULAI 2012
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF, kwa kuzingatia majukumu yake ya kusimamia chaguzi za
wanachama wa TFF kama ilivyoanishwa kwenye Katiba ya TFF, Ibara ya 49 (1), na
Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 26(2) inatoa ufafanuzi ufuatao
kuhusu uchaguzi wa kuziba nafasi za uongozi kwenye Klabu ya Yanga:
1. Wanachama
wote wa TFF, ikiwa ni pamoja na Klabu ya Yanga, wanatakiwa kuzingatia
kikamilifu Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF katika kuendesha shughuli zote za uchaguzi.
2. Wagombea
uongozi wote wa wanachama wa TFF wanapaswa kutimiza masharti ya uongozi
yaliyoanishwa katika Katiba za vyama vyao na Kanuni za Uchaguzi.
3. Kamati
za Uchaguzi za Wanachama wa TFF zinapaswa kutimiza kikamilifu majukumu yao ya
kulinda Katiba za wanachama wa TFF na kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF katika michakato ya uchaguzi. Kamati ya Uchaguzi ya Yanga
ilishaelekezwa kufanya hivyo na inakumbushwa kuendelea kuzingatia wajibu huo.
4. Wagombea
uongozi wa wanachama wa TFF wanao wajibu wa kuzifahamu Katiba zao na Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF na kuomba uongozi kwa kutimiza matakwa ya Katiba
na Kanuni za Uchaguzi.
5. Kamati
ya Uchaguzi ya TFF imepokea maombi ya marejeo (review) dhidi ya uamuzi wake wa
kuwaondoa waombaji uongozi wanne (4) wa Klabu ya Yanga. Kamati ya Uchaguzi ya
TFF inatoa uamuzi ufuatao:
i)
Marejeo yaliyoombwa na Kamati ya
Uchaguzi ya Yanga yanakiuka Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeyakataa. Kamati inafafanua kuwa hata kama Kanuni zingekuwa zinaruhusu kufanya marejeo, bado
maombi hayo yasingepaswa kuwasilishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, bali
waombaji uongozi wenyewe. Pamoja na hayo, sababu za kuomba marejeo si za msingi
kwa kuwa waombaji uongozi na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga walipewa mwongozo wa
kutosha kurekebisha upungufu uliojitokeza katika mchakato wa uchaguzi wa kujaza
nafasi za uongozi kwenye Klabu ya Yanga.
ii)
Sara
Ramadhani hakutimiza masharti ya kuomba uongozi kwa mujibu
wa Ibara ya 10(4) na (5) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na kama
ilivyoanishwa kwenye Fomu namba 1 kwa kutojaza fomu na kutoambatanisha
vithibitisho vya sifa za kugombea. Kwa hiyo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF
inasisitiza uamuzi wake na kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuliondoa jina lake katika
orodha ya wagombea uenyekikiti wa Klabu ya Yanga.
iii)
Shaaban
R. Katwila na Ahmed
Waziri Gao wameshindwa kutimiza masharti ya uombaji uongozi kwa
kutowasilisha vyeti halisi kwa ajili ya uhakiki kama
ilivyotakiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) baada ya nakala za vyeti
vyao kubainika na NECTA kuwa vina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaitaka
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kutekeleza uamuzi wa kuondoa majina yao kwenye
orodha ya wagombea uongozi wa Yanga.
iv)
Ramadhan
Mzimba Kampira ameshindwa kutimiza masharti ya
kugombea uongozi kama
yalivyo kwenye Ibara ya 10(5) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF kwa
kutoambatanisha vithibitisho vya sifa za mgombea. Kwa hiyo, Kamati ya Uchaguzi
ya TFF inasisitiza uamuzi wake na kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuondoa
jina lake katika orodha ya wagombea uongozi.
v)
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaridhia
uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Yanga kuwaondoa wafuatao kugombea
nafasi za uongozi kwenye uchaguzi:
(a)
Ally
Mayay Tembele
(b)
Abdallah
Sharia Ameir
(c)
Jamal
Hamisi Kisongo
(d)
Mohamed
R Mbaraka
vi)
Wagombea uongozi ambao hawakutajwa
hapo juu na ambao walipitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, wametimiza
matakwa ya awali ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na hatua za mwisho
za uhakiki wa vyeti vya elimu yao ,
zinaendelea.
Angetile Osiah
KATIBU
KAMATI YA
UCHAGUZI TFF
0 comments:
Post a Comment