Na Princess Asia
TEMEKE imekuwa timu ya kwanza kupata tiketi ya
kucheza Nusu Fainali kwenye michuano ya mwaka huu ya Copa Coca-Cola baada ya
kuing’oa Mjini Magharibi kwa mikwaju ya penalti.
Mechi hiyo ya kwanza ya robo
fainali imechezwa leo asubuhi (Julai 10 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam ambapo hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo
zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Mjini Magharibi ndiyo walioanza
kupata bao dakika ya 79 lililofungwa na Salum Maulid wakati Abdul Hassan
aliisawazishia Temeke dakika ya 90.
Waliofunga penalti kwa upande
wa Temeke ni Baraka Ntalukundo, Khalid Mwendakamo, Mohamed Dikougwa na Abdul
Hassan wakati aliyekosa ni Anwar Kilemile. Waliokosa kwa Mjini Magharibi ni
Abdulrahman Mohamed na Salum Maulid wakati waliofunga ni Alawi Kombo na Salum
Shukuru.
Katika nusu fainali, Temeke
itacheza na mshindi wa mechi ya robo fainali kati ya Kinondoni na Mwanza
itakayochezwa kesho asubuhi (Julai 11 mwaka huu) Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam.
Robo fainali ya pili ya
michuano hiyo kati ya Mara na Morogoro ilitarajiwa kuchezwa leo jioni kwenye
uwanja huo huo. Mechi nyingine ya robo fainali itakayowakutanisha Dodoma na
Tanga itachezwa kesho jioni.
0 comments:
Post a Comment