Na Princess Asia
TEMEKE imefainikiwa kuilaza Dodoma mabao 2-0 katika mechi ya
kundi C ya michuano ya Copa Coca-Cola iliyochezwa leo (Julai 3 mwaka huu)
kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.
Mabao ya washindi ambao kwa matokeo hayo sasa wamefikisha
pointi tano yalifungwa dakika ya tano Hassan Kabunda wakati la pili lilifungwa
dakika ya 34 na Abdul Hassan.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam umeshuhudia
Morogoro ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Iringa lililofungwa dakika ya
37 na Mutalemwa Katunzi.
Nayo Kilimanjaro imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Tabora katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani. Bao hilo katika
mechi hiyo ya kundi D lilifungwa dakika ya 14 na Eric Christopher.
Kwa matokeo hayo Tabora imebaki na pointi tatu baada ya
kushinda mechi moja tu dhidi ya Pwani, na imebakiza mechi moja dhidi ya Kusini
Unguja ambayo hata ikishinda haiwezi kuingia hatua ya 16 bora.
Nao mabingwa watetezi Kigoma wamejiweka katika nafasi nzuri
ya kucheza 16 bora baada ya kuitandika Kusini Pemba mabao 3-1 katika mchezo wa
kundi A uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko mkoani Pwani.
0 comments:
Post a Comment