Azam Academy, wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa |
Na Prince Akbar
TANZANIA imetawala katika michuano ya Rollingston nchini
Burundi, baada ya kufanikiwa kuingiza timu sita katika hatua ya Robo Fainali ya
michuano hiyo, ambayo awali ilikuwa ikifanyika mjini Arusha.
Timu zilizoingia hatua hiyo ni Azam FC ya Dar es Salaam, JKT
Ruvu ya Pwani, Mjini Magharibi ya Zanzibar, Coastal Union ya Tanga na Bishop
Dunhill na Rollingston za Arusha.
Robo Fainali zote zitachezwa Jumanne katika viwanja viwili
tofauti, Aigle Noir ya Burundi
ikimenyana na JKT Ruvu, Ecofoot ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikimenyana
na Bishop Dunhill Uwanja wa Gisenyi, wakati Azam FC itamenyana na Mjini
Magharibi, Rollingston na Coastal Union Uwanja wa Nyanza.
Mechi za kwanza zitachezwa saa 7:00 mchana na za pili zitachezwa
saa 9:00 alasiri.
ROBO FAINALI ROLLINGSTON:
(Julai 17, 2012)
Aigle Noir (Burundi) v JKT Ruvu
Azam FC v Mjini Magharibi
Rollingston v Coastal Union
Ecofoot (DRC) v Bishop Dunhill (Arusha)
0 comments:
Post a Comment