Taddy wa AS Vita, Azam wachunge sana huyu mtu |
Na Prince Akbar
VITA ya kuwania kiatu cha dhahabu cha Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame imezidi kupambana moto, baada ya Taddy
Etikiama kumpita Said Bahanuzi ‘Spider Man’ wa Yanga kwa bao moja, kufuatia
kufunga kwenye Robo Fainali dhidi ya Atletico ya Burundi leo.
Taddy sasa ana mabao sita, akifuatiwa na Spider Man mwenye
mabao matano, wakati Hamisi Kiiza ‘Diego’hayuko mbali nao sana, akiwa ana mabao
manne, sawa na John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC.
Wachezaji wote hao wanne timu zao zimeingia Nusu Fainali na
wana nafasi ya kuongeza mabao yao, kwani wana mechi mbili zaidi kila mmoja kuelekea
kipyenga cha kuhitimisha Kagame ya 2012.
Wengine waliomo kwenye kinyang’aniyo hicho ni Suleiman
Ndikumana wa APR mwenye mabao mabao matatu, wakati Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’
wa Simba SC timu yake imetolewa leo akiwa ana mabao mawili sawa na Leonel St
Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA.
WANAOONGOZA KWA
MABAO:
Taddy Etikiama AS
Vita 6
Said Bahanuzi Yanga
SC 5
Hamisi Kiiza Yanga
SC 4
John Bocco Azam
FC 4
Suleiman Ndikumana APR 3
Abdallah Juma Simba
SC 2
Leonel St Preus APR 2
Didier Kavumbagu Atletico 2
Feni Ali URA 2
Robert Ssentongo URA 2
0 comments:
Post a Comment