Said Bahanuzi 'Spider Man' |
Na Prince Akbar
MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Said Bahanuzi ‘Spider Man’
yuko hatarini kuikosa mechi ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, Kombe la Kagame kesho dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, kutokana na maumivu
ya mgongo, wakat kiungo Nizar Khalfan yeye kwa asilimia 100 hatacheza kutokana
na maumivu ya nyonga.
Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet ameiambia BIN
ZUBEIRY mchana huu kwamba, Nizar hatacheza kabisa, lakini wachezaji
wengine watatu, Bahanuzi, kipa Yaw Berko
anayesumbuliwa na goti, kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na Hamisi Kiiza wanaosumbuliwa
na quadriceps wako kwenye hatihati kucheza.
Mtakatifu Tom amesema kwamba, Daktari wa Yanga, Sufiani Juma
anaendelea kufuatilia afya za Bahanuzi, Kiiza, Berko na Chuji ili kuhakikisha
wanakuwa fiti kwa ajili ya mechi ya kesho, lakini kwa Nizar kocha huyo wa
zamani wa Namibia na Ethiopia, amekwishakata tamaa kumtumia kwenye mechi na Mafunzo.
Amesema sababu ya wachezaji wake kuumia mara kwa mara ni
kutokana na kucheza mechi mfululizo na kulingana na kanuni za mashindano hayo,
hawezi kutumia wachezaji zaidi ya 20, hivyo hana namna nyingine zaidi ya
kupambana na hali hiyo.
Bahanuzi ndiye kinara wa mabao wa Yanga hivi sasa, hadi sasa
akiwa amekwishaifungia timu hiyo mabao manne, hivyo kuingia kwenye mbio za
kuwania kiatu cha dhahabu cha mashindano hayo, ambayo tayari kwenye kabati la
Yanga kuna mataji manne yamehifadhiwa.
Mshambuliaji huyo mpya kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, juzi
alikaribia kuondoka na mpira uwanjani, kama si refa Dennis Batte kutoka Uganda
kukataa bao lake moja siku ambayo alifunga mawili yaliyokubaliwa dhidi ya APR
ya Rwanda, Yanga ikishinda 2-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Katika mchezo huo, Kocha Tom alimpumzisha Bahanuzi dakika ya
72 na nafasi yake ikachukuliwa na Jerry Tegete, wakati Nizar Khalfan kabla ya
hapo alimpisha Juma Seif ‘Kijiko’.
Wakati huo huo: Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA), leo limesema kwamba mechi ya Yanga kesho itakuwa ya pili, kama
ambavyo itakuwa kwa Simba keshokutwa.
RATIBA ROBO FAINALI
Julai 23, 2012
URA vs APR (Saa 8:00 mchana)
Mafunzo vs Yanga (Saa 10:00 jioni)
Julai 24, July
Atletico vs AS Vita (Saa 8:00 mchana)
Azam vs Simba SC (Saa 10:000 jioni)
0 comments:
Post a Comment