Spider Man; Bahanuzi |
Na Prince Akbar
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Said Bahanuzi ‘Spider Man’
anachuana vikali na mshambuliaji wa AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwenye michuano ya Klabu Bingwa
ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Bahanuzi, aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar msimu huu, ana
mabao matano hadi sasa na mpinzani wake ana matano pia, lakini moja alifunga
kwa penalti kwenye mechi dhidi ya Simba SC.
Ina maana, kama mwendo utakuwa huu hadi mwisho wa siku wachezaji
hao kufungana kwa mabao, basi Bahanuzi atapewa kiatu cha dhahabu kwa sababu hana
bao la penalti, zaidi ya alilofunga lao kwenye mechi dhidi ya Mafunzo katika penalti
za kuamua mshindi baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, ambalo halijaingizwa
kwenye orodha ya mabao yake.
Hamisi Kiiza ‘Diego’, nyota mwingine wa Yanga kutoka Uganda,
anashika nafasi ya pili kwa mabao yake manne, akifuatiwa na Suleiman Ndikumana
wa APR matatu, Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC, Leonel St Preus wa APR,
Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA, wote mabao
mawili kila mmoja.
WANAOONGOZA KWA
MABAO:
Taddy Etikiama AS
Vita 5
Said Bahanuzi Yanga SC 5
Hamisi Kiiza Yanga
SC 4
Suleiman Ndikumana APR 3
Abdallah Juma Simba
SC 2
Leonel St Preus APR 2
Didier Kavumbagu Atletico 2
Feni Ali URA 2
Robert Ssentongo URA 2
0 comments:
Post a Comment