Mrisho Ngassa |
Na Nurat Mahmoud, Renton, Washington
TIMU ya Seattle Sounders FC imetangaza ushirikiano na
Tanzania, nchi ambayo ni nchi kubwa kabisa katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki.Ushirikiano huo ulitiwa saini na Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mheshimiwa Balozi Hamis Kagasheki (Mbunge) na Mmiliki wa timu ya Seattle
Sounders Joe Roth katika hafla fupi iliyofanyika jana mjini Renton.
Mbali ya Waziri Kagasheki, wengine walioshuhudia kutiwa
saini kwa ushirikiano huo ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa
Balozi Mwanaidi S. Maajar, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr.
Aloyce Nzuki na maofisa wengine kutoka
Wizara ya Utalii, Ubalozini na maofisa wa Seattle Sounders FC.
Mambo muhimu katika ushirikiano huo ni uwekwaji wa alama za
vivutio vya utalii vya Tanzania katika maeneo mbali mbali kama CenturyLink
Field na Starfire Sports Complex, uwanja
wa mazoezi wa Sounders FC uliopo eneo la Tukwila.
Vivutio mbali mbali vya Utalii wa Tanzania vitawekwa katika
maeneo hayo kama picha za Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro
Crater na Zanzibar.
"Ushirikiano wetu na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
utasaidia kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania nje ya mipaka yake kwani
kuna vivutio vya ajabu mno na kuleta unafuu kwa watalii ,” alisema Mmiliki wa
timu ya Sounders FC, Joe Roth. Na kuongeza
kuwa ushirikiano huo utatoa nafasi muhimu kwa
soko la Utalii wa Tanzania nchi ya mipaka yake.
Waziri Kagasheki mbali ya kupongeza kwa kufanikisha hatua
hiyo muhimu katika sekta ya Utalii nchini alisema kuwa ushirikiano huo utatoa
fursa nyingi kwa Watanzania na Wamerekani kwani utahimarisha juhudi za Wizara
ya Utalii katika kukuza soko la Utalii wa Kimataifa na wa Ndani.
Mheshimiwa Kagasheki pia alisema kuwa ushirikiano huo utatoa
fursa za kibiashara kwa nchi zote mbili na kuongeza uwekezaji.
Katika kuhakikisha zoezi ujumbe wa kupromoti vivutio vya
Utalii wa Tanzania vinawafikia wengi, michoro mbali mbali ya ukutani itachorwa
kwenye ndani ya uwanja upande wa Kaskazini Magharibi na Kaskazini
Mashariki na itaonekana kwa mara ya
kwanza kwenye televisheni nchini
Marekani wakati wa mechi ya Sounders FC dhidi ya timu ya Chelsea katika uwanja
wa Field CenturyLink Julai 18 (Tanzania Julai 19).
Pia maofisi wa TTB watakuwa mbele wakati wa mkutano wa kabla
ya mechi wa mashabiki wa soka na
kuzungumzia masuala mbali mbali ya utalii na usafiri katika nchi yao.
Timu ya Seattle Sounders FC ilianza majadiliano ya
ushirikiano na Tanzania mwaka 2010
ambapo kocha msaidizi wa timu hiyo Kurt Schmid alisafiri kuja nchini
katika mpango wa kutafuta vipaji vya wachezaji.
Mchezaji wa timu ya Taifa, Mrisho Ngassa kutoka timu ya Azam
FC alisafiri mpaka Marekani na kucheza mechi ya kihistoria kati ya Seattle
Sounders na timu ya Machester United mwaka jana (2011).
0 comments:
Post a Comment